ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, May 28, 2011

Papara ni chanzo cha wengi wengi kufeli kitandani-3GPL

Kila sifa njema anastahili Mwenyezi Mungu. Tunakutana tena leo si kwa ujanja wetu, bali kwa upendo wake. Angekataa tusiwepo, kati yetu hakuna ambaye angekuwa anavuta pumzi leo. Pole nyingi ziende kwa Mchungaji Harold Camping aliyetabiri Mei 21, 2011 ingekuwa mwisho wa dunia lakini haikuwa.

Tuanze mada yetu. Tunahitaji kutibu papara. Tunapaswa kuitambua miili yetu halafu twende na kasi tunayoimudu. Tuache kujipa mizigo tusiyoiweza. Wengi wanakwenda kwa waganga wa jadi wakidhani wanaumwa kumbe ni wazima.


Laiti kila mtu angekuwa mtulivu na kuheshimu hisia zake, naamini waganga wanaotengeneza fedha kwa kuuza dawa za mapenzi au nguvu za kiume wangefulia. Lakini wanapewa jeuri na watu wanaojiuguza ugonjwa wasiokuwa nao.

Zoezi la faragha linatekelezwa kwa nafasi na kituo, si kurukaruka. Umefika mshindo mara hii, baada ya sekunde kadhaa unajing’ang’aniza kurejea ulingoni. Unadhani kwa kufanya hivyo huyo uliyenaye atakuona upo ngangari. Unajidanganya.

Matokeo yake, badala ya kukuona ngangari ndiyo kwanza unaumbuka. Mwili hauko tayari kwa tendo, kwa hiyo papara zako zinakutesa. Unajitesa mwenyewe. Nyama choma ipo mbele yako, unaitamani lakini jeuri ya kuila huna. Aibu!

EPUKANA NA AIBU HII
Achana na simulizi za kijiweni. Usiendeshwe na tamaa. Himili wasiwasi halafu jiamini kwa kila nukta kisha utaona jinsi unavyoweza kutekeleza shughuli ipasavyo. Zingatia kuwa mapenzi yanahitaji muda wa kutosha. Ukitaka kurudi mara mbili ndani ya dakika 15 ndiyo mwanzo wa kuumbuka.

Mtu bora ni yule anayechukua muda kufika mshindo mmoja, halafu anapumzika kwa muda wa kutosha kabla ya kurejea ulingoni tena. Umekutana naye, mara dakika tatu umecheua, kabla hujajipanga unataka upande tutani tena. Utachekwa kila siku.

Imeshaelezwa kuwa mkamia maji hayanywi. Binadamu si kama kilo ya nyama kwamba unaweza kujitutumua na kuimaliza au ukala mpaka ukakinai. Alivyo ni kwamba unapaswa kupata huduma yake na kuridhika ukibaki na tumaini kuwa kesho, wiki ijayo au mwezi ujao unaweza kurudi naye tena ulingoni.

Ukitaka umtumie mpaka huduma yake uikinai shauri yako. Utamg’ang’aniza askari wako afyatue risasi wakati amelala. Papara zako ndizo zitamfanya mwenzi wako aone huna ubavu wa kutosha wakati kumbe ugonjwa upo ndani ya kichwa chako.

KANUNI NI HII
Mtaka vingi kwa pupa hukosa vyote. Hii inapaswa kuwa kauli ya kukuongoza wakati wowote utakapohitaji kuingia faragha ili usiumbuke. Endapo mawazo ya kufunga magoli mengi yataongoza kichwa chako, hata siku moja hutafikia lengo.

Unaweza kupona leo na kuonekana imara kwa mwenzi wako ambaye alishaanza kupoteza imani na wewe. Alishakudharau kwa kuona huwezi tena kumridhisha. Muhimu kwako ni kuacha papara na kuzingatia mambo yafuatayo;

MOSI: Usiogope ukubwa wa samaki, uliza bei yake. Inawezekana anauzwa kwa gharama ambayo unaimudu vilivyo. Muonekano wa nje umekuwa ukiwatesa wengi, unaweza kusafiri kimawazo, ukajikuta umetangulia kitandani kabla mwenzako hajafika.

Inapotokea unakuwa umetangulia kitandani kimawazo kabla ya tukio lenyewe, inakusababishia hisia za kimapenzi ziwe karibu zaidi. Matokeo yake ni kwamba mnapokutana faragha, unakuwa na haraka naye, hivyo kudondosha nanga wakati chombo hakijafika bandarini.

PILI: Usidharau mechi. Usije ukasema huu ni mchezo wa majaribio kwa hiyo usiwe na spidi kali halafu mwingine ndiyo uupangie mashambulizi makali. Hatuendi hivyo, unatakiwa kubeba uzito kwenye kila mpambano. Hutakiwi kuogopa lakini pia usimbeze mpinzani hata siku moja.

TATU: Jiamini na uone mchezo kamili upo ndani ya uwezo wako. Mtathmini mpinzani wako na jenga imani kuwa unammudu kwa sifa zote. Baada ya hapo heshimu shughuli ambayo wewe na mwenzi wako mmekubaliana kuifanya.

NNE: Pumua kwa uhuru. Wazungu wanasema relax. Maana yake ni kwamba unafanya tendo kwa ‘kurilax’. Huna papara, woga wala haraka. Unatekeleza ngwe kwa dakika za kutosha, unajidhibiti usitangulie kabla ya mwenzi wako. Zingatia, mwanamke anapaswa kuanza kufika kileleni au mfike pamoja. Ni kosa kubwa mwanaume kutangulia kileleni.

Ukimaliza mshindo mmoja, pumua kwa wastani. Usielekeze akili yako kwenye tendo ukitaka urejee haraka. Unaweza kumlazimisha ‘swahiba’ aamke, na kweli akaamka lakini utaumbuka kwa sababu nguvu zinaweza kuisha katikati. Jamaa atalala fofofo wewe ukiwa juu ya tuta unalima. Aibu, mpini umesinyaa.

Baada ya mshindo, unaweza kuhamisha mawazo kutoka kwenye tendo. Piga stori za hapa na pale angalau kwa dakika 30 mpaka 45, ikibidi saa nzima ili kuufanya mwili wako upumue kiasi cha kutosha. Ngoja mwili ukwambie kwamba unataka tena halafu rudi ulingoni. Hapo utasherehekea tendo, hutateseka na mawazo, hutajiona mgonjwa tena.

 Wanaoumbuka ni wale wanaotaka kukwea tuta wakati mwili haupo tayari. Wanashambuliwa na hisia za kutaka kushambulia magoli mengi, wakidhani ndiyo wataonekana vidume, matokeo yake huumbuka kabla ya mechi kufika dakika 90.

TANO: Muda ni muhimu. Usipende kujipa muda mchache wa faragha. Mapenzi yanahitaji nafasi, kwa hiyo ni vizuri kabla ya shughuli, uwe umepangiana na mwenzako muda wa kutosha. Hakika wewe siyo mgonjwa ila papara zinakuangusha.

No comments: