ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, May 15, 2011

TEST OF AFRICA MAY 21,2011

 watoto wa Mwangaza Jitegemee Foundation na partner zetu ni (SWACCO) Songea Women And Children Care. Hiki kikundi kipo Songea Mkoa wa Ruvuma Chini ya Mkurugenzi Regina Chinguku na wasaidizi wake Mama Lupogo, Giftyness. Mwenyekiti wa Board ya SWACCO ni Albert Kessy. Watoto18 wanaishi ndani ya nyumba ya Regina na Alkun Chinguku Tangu 2003 kwa sasa wamekuwa wakubwa wanahitaji nafasi zaidi. Kiwanja tumenunua, Ramani imechorwa na wataalam kutoka hapa Marekani na imekaguliwa na wataalam wa sheria za majenzi ya Tanzania mkoa wa Ruvuma ikisimamiwa na Erick Mapunda. SWACCO ina eka 31 mpaka sasa kwa mahitaji ya watoto Yatima. Ramani imekubalika na Serikali ya Tanzania.Baadhi ya matofali tumekwisha piga, Kisima kimoja tumechimba na mwezi huu tunachimba kisima kingine kikubwa zaidi, tunategemea kitasaidia kituo cha watoto na pia kitanufaisha wananchi waishio ktk maeneo hayo.  Kisima hiki kitachimbwa na Khamis Drima Mat and Groundwater Services LTD akisimamiwa na  wataalamu kutoka Amerika na Japan. Na tutatoa ajira fupi kwa wananchi ikiwepo Elimu ya upigaji matofali kwa kutumia mashine za kisasa.

Mwangaza Jitegemee Faundation tunategemea kutafuta michango mbalimbali ndani na nje ya America. Kwa kufanikisha mradi huu tunawakaribisha watu wote wenyekujisikia kuchangia au kujifunza zaidi kuhusu Mwangaza Jitegemee Foundation kutembelea Songea na kuonana na watoto pamoja na wanawake wa SWACCO au tembelea www.mwangazajitegemee.org or facebook ya mwangazajitegemee.

No comments: