Advertisements

Tuesday, May 3, 2011

Uswizi yapiga tanji mali za Gaddafi

Muammar Gaddafi
Uswizi imesema imepiga tanji takriban mali zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni moja za Kanali Muammar Gaddafi wa Libya na viongozi walioondolewa madarakani kutoka Misri na Tunisia.

Waziri wa mambo ya nje wa Uswizi Micheline Calmy-Rey alisema takriban dola za kimarekani milioni 960 zimepatikana.
Waziri huyo alisema, kati ya hizo, kiwango kikubwa cha faranga za kifaransa milioni 410 zimehusishwa na aliyekuwa Rais wa Misri Hosni Mubarak na washirika wake.
Faranga nyingine zenye thamani ya milioni 360 zinaaminiwa kuwa za uongozi wa Kanali Gaddafi.
Na faranga milioni 60 zinamhusu aliyekuwa kiongozi wa Tunisa Zine al-Abidine Ben Ali na washirika wake.

No comments: