Monday, May 2, 2011

Wengi wanapoteza mvuto, wanaachwa kwa sababu hawajitambui-2(GPL)

Wiki iliyopita niliishia kumwelezea mtu aliyekuwa anasumbuliwa na tatizo la kukimbiwa na wapenzi. Ukweli ni kwamba jamaa aliteseka lakini baada ya kujua kiini cha tatizo, mara moja alitafuta njia za utatuzi.


Baada ya kuachwa na wapenzi wanne kwa mtindo wa kila aliyefanikiwa kuingia naye faragha kutorudi tena, alikuja kubaini kuwa kumbe kilichomtesa ni ukubwa wa umbile lake la siri (nyeti).

Huyu jamaa niliwahi kuzungumza naye, akanimbia: “Wakati wa tendo, mwanamke analia kwa nguvu sana. Mmoja amewahi kuning’ata wakati nalazimisha kuingia ndani.” Alinionesha alama ya kung’atwa kifuani. Nilimhurumia kwa sababu nilimsoma machoni kwamba tatizo hilo lilimtesa.

NIlichomshauri; yeye si mgonjwa. Ni mzima kwa asilimia 100. Wapo wanaoteseka kutokana na maumbo yao madogo ambao nao husimangwa kwamba hawawafikishi kokote wenzi wao wanapokutana faragha. Sasa iweje yeye makubwa yamnyanyase mpaka akose amani?

Njia niliyompa: Kwanza hatakiwi kuwa na papara anapokutana na mwanamke faragha. Ajitahidi kwenda naye taratibu kwa kadiri inavyowezekana. Nilimwambia hivyo kwa sababu niligundua kwamba kikubwa kilichokuwa kinamsumbua ni papara za mchezo.

Nilimweleza kuwa wanawake walivyoumbwa, maumbile yao huongezeka kulingana na kile ambacho wanakipokea. Hii ina maana kuwa, umbo kubwa la ndugu yetu si tatizo ikiwa tu atakuwa na nidhamu wakati wa tendo. Hata kama ni umbo dogo, bila maandalizi bado mwanamke anaweza kupata maumivu makubwa.

Nilimwambia atulie, amwandae mwenzi wake mpaka awe tayari, baada ya hapo ndipo anaruhusiwa kuingia mchezoni lakini kwa taratibu. Si kwenda pupa, matokeo yake anamuumiza mtoto wa mwanaume mwenzake mpaka akome kumfahamu. Huyo akiondoka harudi!

Mwezi mmoja baada ya kumshauri kitu cha kufanya, jamaa yangu huyo alirudi kunishukuru. Alikuja akiwa mwenye furaha. Aliniambia: “Kweli nimekubali, mwenzangu niliyenaye sasa ni yule ambaye mwanzoni alijiapiza kurudi kwangu kwa madai eti nilimuumiza sana.

“Siku ile baada ya kutoka kuzungumza na wewe, nilikwenda kwao, nikamuomba lakini alikataa mpaka nilipomweleza kuwa nimeongea na mshauri na amenipa njia za kufanya, hivyo sitamuumiza tena. Kimsingi alinikubalia lakini ilikuwa ni kwa shingo upande.

“Mara ya kwanza tulipoingia faragha, alionesha ana wasiwasi mwingi. Hilo nililijua, kwa hiyo nilijitahidi kwenda naye kistaarabu. Nilimwandaa kisaikolojia mpaka akabadilika, baada ya hapo nilimwandaa kwa tendo, akanyooka na kuashiria yupo tayari kwa chakula.

“Nilikwenda naye taratibu, alipokaribia kileleni, nilienda naye na kufika pamoja. Alifurahi sana. Mwanzoni alidhani nimebahatisha lakini tuliporudia tena, nilikwenda naye kwa utaratibu ule ule na akawa kweli ameridhika.

“Hiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kusifiwa na mwanamke kuwa nimempa raha na amefika kileleni. Mwanzoni nilijiona nina mkosi na sina ujanja wowote mbele ya wanawake. Hivi sasa mwenzangu yupo tayari tufunge ndoa. Ameridhika kuwa na mimi kwa maisha yake yote, kwa maana kila tunapoingia faragha, anafika anapopataka na hilo ameshanihakikishia mara nyingi.”

Kimsingi jamaa alinishukuru sana lakini nilichompa hakikuwa uchawi au jambo lenye maajabu. Nilimpa ukweli halisi wa kisaikolojia kwa maana nzima ya dhana ya kujitambua. Ikiwa hujitambui, maana yake utabaki kwenye kasoro ile ile kila kukicha na hutaona matunda.

Unaachwa na wapenzi mara kwa mara, badala ya kujitazama ili utambue kasoro uliyonayo, wewe unakimbilia kuamini kwamba umerogwa au umeumbwa na mkosi. Ndugu yangu, hata siku moja usije kujidanganya, Mungu hakumuumba binadamu na nuksi.

Pengine wewe ni mchafu. Unapoingia faragha na mwenzi wako, unageuka karaha kutokana na kutoa harufu kali. Inawezekana huuandai mdomo wako vyema, hivyo unatoa harufu kali. Mwenzi wako anashindwa kuwa huru kuongea na wewe kwa ukaribu. JItambue.

Itaendelea wiki ijayo.

No comments: