ANGALIA LIVE NEWS

Friday, June 3, 2011

Mpe uhuru mpenzi wako, akupe penzi kamil-GPL

MUHALI gani mabibi na mabwana ambao mpo ndani ya ndoa au kwenye uhusiano wa kimapenzi usio rasmi, kwa uwezo wa muumba nina imani ni wazima wa afya na ndiyo maana tupo pamoja katika mada yetu.

Leo napenda nizungumzie uhuru ndani ya mapenzi, unamfanya mtu ajiamini na kukupa penzi kwa asilimia 100 bila woga. Najua unajiuliza ni uhuru gani huo ndani ya mapenzi?


Katika uchunguzi wangu nimepata malalamiko mengi toka kwa wanawake ambao siku zote hufanywa chombo cha starehe na kunyimwa uhuru wa kuzungumza wakati wa mapenzi, hufikia hatua hata kama amechoka anaogopa kusema kwa kuwa atakalipiwa au kuambiwa alikuwa na mwanaume mwingine muda mfupi kabla ya hapo. Ooh! Hapana haiendi hivyo.

Mapenzi ni
makubaliano si ubabe:
Mapenzi si ugomvi, ni raha za upande mmoja, unapojisikia lazima utimiziwe hata kama mwenzio anaumwa. Hufanya hata mwanamke apoteze hamu ya mapenzi kila akuonapo. Hii humfanya hata mnapokuwa kwenye dimbwi la mahaba anakuwepo tu na si kulifurahia penzi bali kutimiza haja ya mumewe au mpenziwe.

Nini maana ya mapenzi?
Mapenzi maana yake ni upendo, furaha, tulizo la moyo na kato la kiu ya mwili, raha za pande mbili, kuoneana huruma n.k. Mfanye mpenzio alifurahie penzi lako, alikumbuke hata uwapo mbali.

Ili mpenzi wako aweze kufurahia penzi lako, lazima umpe uhuru ili akupe penzi lake toka chini ya uvungu wa moyo wake, mfanye alie kilio cha furaha siyo cha maumivu. Wewe na mpenzio kila mmoja ana uhuru wa kufanya atakavyo katika mwili wa mwenzie bila kuvuka mipaka wala kulazimishana bali kwa kuridhiana, kitu kinachofanya kila mmoja ajisikie raha na furaha.

Kila kiumbe kina udhaifu wake hasa mnapokuwa kwenye mapenzi, wapo wanaolia utafikiri wameonewa kumbe raha zimewazidi, baadhi huongea kama wamemeza CD ya maneno, wengine utafikiri si muda mrefu atakata pumzi, mwingine jicho kiini cheusi hakionekani, yote hayo ni kutokana na kuwa huru na kuweza kushughulika bila woga.

Ifike hatua wanaume tubadilike, Oooh nimekumbuka kuna mtu kanitonya eti wanaume wengine huwa wakali kwa kuwa mambo mengi ya mahaba hawayajui. Lakini nina imani kupitia kona hii tutaelemishana na kukufanya ulifurahie penzi bila ngumi wala lugha kali.

Hakuna aliyezaliwa anajua, wote wamejifunza kupitia njia hizi au kuuliza kwa wenzao, usione aibu kuuliza, nina imani kama utakayemuuliza anajua na akiwa siyo mchoyo atakupa darasa.

Elimu hii ni ya bure, mpe mwenzio naye ajikute siku moja chozi likimtoka kwa raha za ajabu ambazo hajawahi kuzipata. Nina imani nimeeleweka tukutane wiki ijayo kwa mada mpya nakutakieni mapenzi matamu yenye utamu yasiyoisha hamu.

No comments: