Serikali ya Zimbabwe imemfukuza balozi wa Libya nchini humo ambaye wiki iliyopita alimuasi Kanali Muamamar Gaddafi na kuwaunga mkono waasi.
Taher Elmagrahi alijiunga na waandamanaji waliovamia ubalozi wa Libya mjini Harare na kupeperusha bendera ya waasi katika afisa za ubalozi mjini Harare.
Lakini Waziri wa mambo ya njee ya Zimbabwe amesema wao hawaitambui baraza la mpito la Libya .
Rais Robert Mugabe ni rafiki mkubwa wa Kanali Gaddafi ambaye alikuwa akiifadhili Umoja wa Afrika. Na ni mataifa machache ya Kiafriak ambayo yameitambua Baraza hilo la mpito la Libya.
Wiki iliyopita Serikali ya Zimbabwe ilipinga hatua ya Baraza la Umoja wa Mataifa la kuruhusu waasi wa Libya kupewa persa za serikali ya Libya.
Waziri wa Mambo ya Njee wa Zimbabwe Simbarashe Mumbengegwi ambaye ni wa chama cha Zanu-PF kinachoongozwa na Robert Mugabe amesema kuwa balozi huyo ana saa 72 pekee yake kuhama nchi.
"mara tu unapoasi mamalaka yaliokuchagua na kukua uwezo wa kuwa balozi na kuaanza kutii amri za watu wengine ... Inamaanisha kuwa tendo hilo linakupokonya haki ya kutambulika kama balozi", alisema
na juma lililopita alipotangaza kuunga mkono waasi bwana Elmagrahi alisema kuwe yeye sio balozi wa Gddafi ." nawakilisha watu wa Libya"
wanahabari wanasema kuwa Rais Mugabe na wapambe wake wanawasiwasi sana kufuatia mapindulizi yaliotokea nchini Libya.
Wanaharakati 40 walikamatwa mapema mwezi wa Februari baada ya kupatikana wakitazama video kuhusu mapinduzi ya Misri.
Bwana Mugabe ameishutumu NATO kwa kuingilia Libya akisema kuwa vita hivyo vilikuwa ni kwa sasabu ya mafuta.
No comments:
Post a Comment