
Katika kuanza sehemu ya pili ya makala haya, ni vema kupeana muongozo kwamba maisha ya uhasama hayatakiwi kwa namna yoyote. Kuna mambo mengi ya kushughulikia kwa ajili ya maendeleo binafsi na taifa kwa jumla.
Una muda mwingi kiasi gani? Kukaa na chuki na mwenzako ni ishara ya kutokuwa na kazi za kufanya. Hutakiwi kuonekana huna mambo ya kushughulikia. Badilika leo, ondoa kinyongo kwa kila uliyetofautiana naye. Ukizingatia huu ni Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Una muda mwingi kiasi gani? Kukaa na chuki na mwenzako ni ishara ya kutokuwa na kazi za kufanya. Hutakiwi kuonekana huna mambo ya kushughulikia. Badilika leo, ondoa kinyongo kwa kila uliyetofautiana naye. Ukizingatia huu ni Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Kaa na ufahamu kwamba ni kazi ngumu kumchukia kila mtu. Lazima ukubali kuwa maisha ni safari ndefu, utagombana na mpenzi wako leo, inawezekana kesho ukatofautiana na wengine. Swali la kujiuliza ni moja, je, utakuwa na maadui wangapi kabla hujaingia kaburini?
Unahitaji amani na furaha. Utulivu wa moyo wako ni jambo muhimu katika kuhakikisha unapiga hatua za maendeleo. Tambua kwamba mtandao wa maadui ni hatari iwapo utakuwa unataka kutimiza azma yako. Ongeza marafiki, punguza maadui.
Kuna kitu kizuri ambacho nimeona nikufumbue. Mwenzi wako wa zamani anapogundua unamchukia, huona fahari kwamba anayagusa maisha yako, hivyo anaweza kuichezea akili yako kadiri anavyoweza. Nawe utaumia kwa sababu yupo ndani yako.
Anaweza kukupiga vijembe au kukatiza mbele ya macho yako na mpenzi wako, lengo lake ni kukuoneshea. Anajua utaumia na kweli utaumia. Hili ni kosa, kwa hiyo unatakiwa kupotezea historia ya zamani. Angalia macho yako. Ukimuona usinune wala kuonesha umeshtuka.
USIMPONDE
Kuna uwezekano ninyi wawili mlikuwa hamuendani. Hilo unalikubali ndani yako kwamba vitu vingi mlitofautiana. Hata hizo siku ambazo mlikaa pamoja, maana yake mlijitahidi kwa kila hali kuvumiliana na kulazimisha mapenzi.
Hata hivyo, hiyo haina maana kutangaza kwamba alikuwa haendani na wewe. Kufanya hivyo ni matumizi mabaya ya muda wako. Mungu aliyekuumba anahitaji ujitume kusaka maendeleo yako na familia kwa jumla.
UNAWEZA KUMKOSEA MWENZI WAKO
Fikiria kuwa umeachana naye na sasa upo na mwingine. Huyu mpenzi wako mpya anagundua kwamba unamchukia aliyepita. Kama ni mjanja, atajua bado unampenda ndiyo maana hajakutoka moyoni.
Mantiki ni kwamba kitu kinachokuumiza maana yake kinakugusa, kwa hiyo mpenzi wako mjanja ataanza kuwa mbali na wewe, kwani atahisi bado mapenzi yako yapo kwa mtu wako wa zamani, kwa hiyo atashindwa kuwekeza muda wake kwako.
Atakuogopa, atajua siku mkiamua kuyamaliza yeye atabaki njia panda. Busara ilale sehemu yake na ni vema ukazingatia ukweli kwamba kukaa na chuki na mtu wako wa zamani ni kumkosea heshima mwenzi wako wa sasa.
KILA SIKU TAZAMA MBELE
Siku zote, kikomo chako cha kufikiri kikupeleke kwenye eneo kwamba ni lazima umsahau mwenzi wako wa zamani. Huhitaji kubeba mizigo isiyobebeka. Angalia usifanye kitu cha kumfanya ajue kuwa umeathirika na kutengana kwenu. Hiyo inampa sifa kubwa na atajifagilia hata kwa marafiki zake.
Kisaikolojia ni kwamba chuki huja baada ya hisia kuwa uhusiano wako ulikuwa ni muhimu sana, ulitamani muendelee kuwa pamoja lakini imeshindika. Inamaana umekwazika kumpoteza. Hujui tu, lakini mwenzako unampa kicheko na anajiona mshindi.
Wewe unamuwaza lakini yeye hana muda. Anafanya mambo yake kwa raha zake. Tafadhali, usifike huko. Hisia za kuamini kuwa uhusiano wako utaendelea kudumu ni kosa kubwa. Acha aende, maisha ni matamu bila yeye.
SIKU ZOTE ZINGATIA HAYA
Unaachana na mwenzi wako leo zingatia mambo yafuatayo ili yakusaidie kuishi kwa amani.
1. Komesha mawasiliano yote naye.
2. Achana na hisia kuwa kuna siku wewe na yeye mtarudiana.
3. Fanya mambo chanya kwa ajili ya maisha yako, soma kuongeza ujuzi, itakusaidia.
www.globalpublishers.info
No comments:
Post a Comment