Au mathalani mtoto anaweza kutenda kosa, mzazi mmoja anaamua kumwadhibu, lakini upande mwingine wa mzazi anaona adhabu hiyo hakustahili kupewa na kuamua kuingilia kati, utakuta badala ya kumwadhibu mtoto matokeo yake wao ndiyo wanaanza kuadhibiana.
Migogoro mingine ambayo husababishwa na watoto kwa wana ndoa, ni uchonganishi kwa wazazi. Mfano mama anafanya kosa fulani mbele ya mtoto wakati baba akiwa hayupo nyumbani, lakini baba akirejea, mtoto anaanza kumweleza kila kitu, hivyo kwa uchonganishi huo kama baba hatatumia busara, basi migogoro huweza kuibuka.
Migogoro mingine ambayo husababishwa na watoto kwa wana ndoa, ni uchonganishi kwa wazazi. Mfano mama anafanya kosa fulani mbele ya mtoto wakati baba akiwa hayupo nyumbani, lakini baba akirejea, mtoto anaanza kumweleza kila kitu, hivyo kwa uchonganishi huo kama baba hatatumia busara, basi migogoro huweza kuibuka.
WATOTO HUDIDIMIZA UCHUMI!
Hili liko wazi kuwa wingi wa watoto katika familia huchangia kudidimia kiuchumi.
Watoto wengi kuanzia umri wa miaka 15 kushuka chini, huwa hawawezi kuingiza pato lolote kwenye familia zaidi ya kuhudumiwa kila kitu, hali hii husababisha wazazi kutumia kipato kikubwa kwa kuwahudumia na kushindwa kufanya mambo mengine muhimu katika kujikwamua kujiletea maendeleo.
Hivyo watoto hudidimiza uchumi katika familia wanapokuwa bado katika umri wa kuhudumiwa kila kitu. Ndiyo maana utakuta wanandoa wanafikia uamuzi wa kuzikimbia familia (hasa akina baba) kwa kuzidiwa na wimbi la kiuchumi.
MUHIMU ZAIDI
Ndugu msomaji, zipo hasara nyingi za watoto kimapenzi katika ndoa, lakini kwa uchache hizi zinatosha kuonesha ni kwa jinsi gani watoto huleta adha katika ndoa. Jambo la muhimu kuzingatia hapa ni kwamba, kila mzazi ajue wajibu na majukumu yake kwa mwenzake na uwepo wa watoto katika ndoa usiwe chanzo cha kupunguza na kusitisha huduma muhimu kwa mwenzako katika ndoa.
ANGALIZO
Pamoja na hasara za watoto kimapenzi katika ndoa, lakini pia watoto ni muhimu sana katika ndoa, kwani huchangia kukuza furaha katika familia na ndoa kwa ujumla, hivyo basi suala la kuzingatia katika hili ni kuwalea katika misingi bora ya kimaadili, na kila mwanandoa kuzingatia mipaka, majukumu na wajibu kwa mwenzi wake pia kutoruhusu watoto wabomoe misingi mizuri ya mapenzi mliyokuwa nayo hapo awali.
Nakutakia afya njema na zingatia haya machache. Tuonane wiki ijayo kwa mada nyingine nzuri zaidi
www.globalpublishers.info
No comments:
Post a Comment