ANGALIA LIVE NEWS

Friday, August 26, 2011

JUMLA YA DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI 777 ZIMETENGWA KUKAMILISHA MPANGO WA UNDAP 2011-2015.

Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Alberic Kacou akifungua rasmi semina ya waandishi wa habari na wataalamu mbalimbali wa mashirika ya Umoja wa Mataifa Tanzania nchini,  juu ya mpango kazi maalum wa miaka minne unaojulikana kama United Nations Development Assistance Plan 2011-2015 (UNDAP) Semina imefanyika kwenye Hoteli ya Movenpick jijini Dar es Salaam.
 Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu akiwakaribisha wadau na waandishi wa habari katika semina hiyo.
 Mratibu wa Ukuaji Uchumi kutoka FAO Dkt. Vedasto Rutachokozibwa akibadilishana mawazo na waandishi wa habari katika Semina ya UNDAP iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Afisa Uhusiano wa UNHCR Juliana Bwire akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mpango mzima wa UNDAP kwa upande wa sekta ya wakimbizi ambayo Mwakilishi Mkazi wa UN nchini Alberic Kacou amesisitiza ushirikiano wa pamoja kati ya Serikali ya Jamhuri ya Tanzania na Umoja wa Mataifa.
Mtaalamu wa Masuala ya Kulinda Haki za Watoto wa UNICEF Mona Aika akitoa maelekezo kwa Mwandishi wa habari wakati wa semina ya mpango kazi maalum wa miaka minne unaojulikana kama United Nations Development Assistance Plan 2011-2015 (UNDAP).
Mmoja wa watumishi wa IAGG Bi. Salome Anyeti akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya masuala ya Haki na Jinsia katika mwendelezo wa semina iliyoandaliwa na UN Tanzania kwa lengo la kuhamasisha waaandishi wa habari kuandika na kuelimisha jamii juu ya mpango wa MKUKUTA  na MKUZA  kwa kipindi cha miaka 4 ijayo. Kushoto ni Bw. Robert Basil Mwenyekiti wa IAGG upande wa Jinsia na Maambukizo ya Ukimwi kutoka kitengo cha Chakula na Kilimo UN.
Afisa Program wa WFP Said Johari na Afisa Uhusiano wa michango wa WFP Fizza Moloo wakizungumza na mwandishi wa habari alitembelea kitengo hicho wakati wa semina ya mpango kazi maalum wa miaka minne unaojulikana kama United Nations Development Assitance Plan 2011-2015 (UNDAP).

www.mohammeddewji.com/blog

No comments: