Kwanza kabisa, nakupa pongezi Luke kwa juhudi na moyo wa kujitolea
mara zote ili kutuletea habari na matukio kwa wana DMV kila siku. Ni heri
kukusifia leo na kukupongeza sasa ili uendelee kufanya zaidi. Katika hili
nasema Mungu akubariki sana na kukulipa baraka nene.
Jambo la pili ni kwamba nashukuru sana kwa historia ya wanaDMV aliyoitoa
mzee Kalala kupitia VIJIMAMBO. Mimi binafsi nilikua sijui kabisa historia hiyo na kwa
nini jumuiya haikuwa na uhai hadi leo kiasi cha kufa na kutafuta kuifufua tena. Ni kweli kwamba
utendaji wa kujitolea ni mgumu sana hasa ukizingatia mtu aongozaye anamajukumu yake
ambayo ni namba moja. Utendaji wa jumuiya utamsubiri kiongozi huyu akiwa na muda wa
ziada tu, akikosa basi. Nionavyo mimi ktk jambo hili, kama tutafufua jumuiya basi suala
la uongozi liangaliwe upya.
Mwisho napenda kuwaomba wanaDMV wote hasa kwa mujibu wa maoni ya mzee
Kalala kwamba waliomba marekebisho wako wapi? Je waliomba kwa kumaanisha au la!
Kama kweli maoni ya kurekebisha katiba walitoa watu watatu tu ni dhahiri kwamba wana
DMV hatuna haja ya kuwa na jumuiya. Lakini alama za nyakati zinasema wenzetu wa majimbo
mengine wanazidi kupeta ki-jumuiya sisi tunaumana na kutafunana wenyewe. Jambo hili sidhani
linahitaji kuchukuliwa kama la kawaida, ni nyeti sana kwa maendeleo yetu na watoto wetu na
hata taifa letu. Wana DMV tupatikane kirahisi wajemeni kwenye maoni na ktk mikutano ya DMV.
ASANTE SANA DJ LUKE,
Rev: Malekela MJ.
MSIKILIZE MZEE KALALA
3 comments:
Mzee Kalala umesema ukweli; siku zote nimekuwa nikiamini jumuiya hii inaweza kurudi ikiwa tu wazee waasisi wa DMV wataungana pamoja kwenye kuifufufa. Siamini hata siku moja kama ubalozi utaweza kuifufufa jumuiya hii. Viongozi waliopo ubalozini wanamajukumu makubwa ya kulitumikia Taifa letu, ubalozi unachoweza ni kuratibu kama alivyojaribu mama Majaar. Mzigo wa jumuiya hii ni wetu watanzania wa DMV. Si lazima kila mtanzania awe mwanachama. Ipo haja ya kutofautisha kati ya utanzania na mwanachama, hili ndilo tatizo kubwa lilosababisha wapo watanzania wanaoaminikuwa kila mtanzania ni mwanachama lakini cha ajabu hawataki kuiheshimu katiba. Ninachosisitiza jumuiya ni chombo cha hiyari wale ambao hawaoni umuhimu wa chombo hiki wangejiweka pembeni tutaendelea kusaidiana nao kama watanzania. Ombi binafsi kwa wazee, rudisheni mioyo yenu. Wengi mlivunjiwa heshima zenu upo msemo unasema MTU MZIMA JALALA; wasemeheni vijana ili tusonge mbele.
Mzee umeongea busara sana hasa ulipohoji mtu unapochagua kiongozi unataka kuongozwa kwenda wapi? Hili ndilo swala linaloua jumuiya nyingi tu popote duniani. Malengo ya jumuiya zetu bado yanafuta miongozo ya ujamaa na kujitegemea, na misiba ndio imekua lengo kuu la jumuia. Jumuia ya leo sharti izingatie changamoto za maisha ya leo. Jumuia ilenge mambo yote ya kijamii yanayotuhusu kama birthdays, graduations, anniversary, appointments, business and many more. Tuwe na jumuiya inayotukutanisha kwa mengine, misiba isiwe kichwa cha habari. Sasa mtu ameoa/ameolewa mtu wa taifa jingine halafu unamwambie kila weekend twende kwenye mkutano wa jumuia ya msiba, manake nisipoenda sitarudishwa kwetu kuzikwa, atakuelewa? sio kweli watanzania wa DMV hawapendi umoja ila viongozi waliopita wamewavunja mioyo ndio maana tunahitaji sura mpya zenye uwezo wa ku implement road map yenye mvuto.
Kwanza kabisa nakubaliana na yote alitoyaeleza mchangiaji Anonymous wa August 7, 2011 8:54PM. Ningependa kuongezea kwa kusema kuwa mie ni mkazi wa Washington DC kwa zaidi ya miaka ishirini. Mzee Kalala amegusia tu dalili za ugonjwa (symptoms) wa jumuia ya watanzania Washington DC (JWW). Hakutoa kiini cha matatizo yake.
Matatizo ya JWW yalisababishwa na yameendelea kusababishwa na viongozi wabadhirifu, waliokuwa wanapokea michango ya watu (tena walio henyea kazini vibaya vibaya). Hao viongozi waanzilishi na wengine walio fuata (majina kapuni) walikuwa wanatumia jumuia kama kitega uchumi chao cha kulewea na kuwasaidia nyumba ndogo zao. Ilikuwa vilevile kuna kupeana uongozi wa makundi hayo hayo, hivyo ilikuwa vigumu kufanya mabadiliko. Hii ilipelekea kwamba wanachama watarajiwa na wale tuliokuwapo kuacha kuamini mambo yote ya chama.
Baada ya kuona kuwa chama hakiendelei na wanachama hawachangi, kuna uongozi fulani (jina kapuni) ulianza kupitia kwenye misiba na kumwambia mfiwa nyumbani kwake kuwa "unaona umefiwa.. ungekuwa mwanachama tungekusaidia kusafirishia"... Hata kama ni kutafuta wanachama njia hii ilikuwa inakera sana na inaenda kinyume na utamaduni wetu wa kitanzania.
Kwa kifupi, JWW ilianzishwa kwa misingi isiyo mipana (kama alivyoeleza anonymous hapo juu), ilikuwa na viongozi walevi na wahuni, walikuwa hawana mipango makini ya kuikuza jumuia na kuiendeleza.
Kuna taasisi nyingi sana na zinazofanya mambo makubwa na bado zinazoendeshwa na viongozi wanao jitolea muda wao.. Hasa hapa marekani. Hili suala la malipo ni kisingizio na nimiongoni mwa tabia mbaya ya kutojituma kwa watanzania(nitaeleza baadaye). Hivi hao viongozi wanapo gombea hizo nafasi hawajui kuwa ni kazi ya kujitolea na kwamba itabidi wawe na muda ? Taasisi iongozwe na wanaolipwa kwa michango ya uana chama ? There has to be a better model... may be income generating model ili kwamba kuwalipa viongozi kuwe sustainable... This means inabidi wawe viongozi walio soma na wana elimu ya kupambanua haya...leadership should be merit based over and beyond just kupigiwa kura. Na viongozi wawekewe malengo kila mwaka wasipo weza ku-deliver wanafukuzwa. Huo ndio mfumo unaweza kufaa kwa viongozi wa kulipwa, lakini usajili wa chama uendane na model hii.
Watanzania inabidi tuamke na tuweze kuaona mambo kwa mtazamo mpya.
Watanzania wanataka ama kulipwa kwa shughuli zinazo wanufaisha wao ama wasilipe kupata huduma eti kwavile ni watanzania. Mfano ni mkusanyiko wa DICOTA, watanzania wengi wanahoji kwanini wachangie... Naona hata aibu kuzungumzia jambo hili la kutochangia kushiriki DICOTA.
Kinyume na Mzee Kalala, tatizo la JWW halitotatuliwa na kulipwa viongozi kwa michango ya wanachama na wala ofisi ya ubalozi. (Ubalozi unaweza kuratibu tu..). Tatizo la JWW kwa mfumo huu wa michango pekee...lita tatuliwa na viongozi wenye nia ya kukiendeleza chama, na sio viongozi wanotafuta namna ya kudokoa(kipato kidogo sana) kwa kutumia social issues za misiba katika jamii.
Na mchango wangu katika hili ni kwamba chama hiki kingeendeshwa kwa michango ambayo inawekezwa na kutoa faida.. hii tu ndio jinsi inatayowezesha kiongozi kulipwa.. na kama itakuwa hivi inabidi chama kisajiliwe tofauti, viongozi wawe wasomi, wanaopewa majukumu na malengo yanayo pimika. Ili kufanikisha hili, inabidi wadau wachache sana waanze hata bila wengine na matokeo mazuri yatawavuta wengine kujiunga... This is the only way JWW can prove itself again... Kimepakwa matope sana na uongozi mbaya ulio kianzisha..
Ahsante
Post a Comment