Na Luqman Maloto
Tupo kwenye Mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Leo ni chungu cha 14. Jumatatu tutakuwa tunazungumzia habari ya kuugawa mwezi. Namshukuru Mungu kwamba tunaendelea kukutana kwa njia ya maandishi. Mimi naandika, wewe unasoma, hakika Mungu ni mtakatifu kweli kweli.
Tuanza mada yetu msomaji wangu: Si ajabu hapo ulipo ukawa na mawazo tele. Unajiuliza kwa nini hupati mchumba. Watu wa rika lako uliokua nao, hivi sasa wanajenga familia zao, wewe bado unakomaa na maisha ya usimbe au bachela (neno la kutohoa kwenye Kiingereza.
Tupo kwenye Mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Leo ni chungu cha 14. Jumatatu tutakuwa tunazungumzia habari ya kuugawa mwezi. Namshukuru Mungu kwamba tunaendelea kukutana kwa njia ya maandishi. Mimi naandika, wewe unasoma, hakika Mungu ni mtakatifu kweli kweli.
Tuanza mada yetu msomaji wangu: Si ajabu hapo ulipo ukawa na mawazo tele. Unajiuliza kwa nini hupati mchumba. Watu wa rika lako uliokua nao, hivi sasa wanajenga familia zao, wewe bado unakomaa na maisha ya usimbe au bachela (neno la kutohoa kwenye Kiingereza.
Kama mwanamke, taratibu unaanza kuwa mnyonge. Upweke unakusumbua, kwa mbali unashawishika kuwa kuna mkono wa mtu katika tukio lako la kukosa mwanaume ambaye amehitaji kukuoa.
Kundi hili la wanawake ambao wamekaa muda mrefu bila kuolewa huhisi wana upungufu mkubwa kwenye jamii, hivyo huamua kwenda kwa waganga wa kienyeji kama sehemu ya kutafuta dawa ya tatizo la kukosa waume wa kuwaoa.
Wanaokwenda kwa waganga wa kienyeji hupoteza njia. Wanapaswa kuchunguza hulka zao. Sangoma hana ubavu wa kumpa mtu dawa ili akikatiza barabarani wanaume wawe wanamuangalia kwa jicho la kutaka kumuoa.
Hata kwa mwanaume, japo si sana kutokana na asili ya maumbo yao kuwabeba lakini bado na wao wakati mwingine hujikuta wanazeeka bila kuwa na wake kutokana na hulka zao. Mada hii ina majibu ya kile kitu ambacho kwa namna moja au nyingine kilikuwa kinakuumiza kichwa kuhusu ndoa.
Jambo ambalo ni vema kila mtu akalijua ni kuwa ndoa ni mtu mwenyewe. Jinsi ambavyo wewe mwenyewe unajiweka ndivyo unavyoweza kuolewa au kupata mke wa kuoa mapema. Ukiwa macho juu unadhani nani atakubali ujiweke kwake?
Naishi kwenye jamii kama yako msomaji wangu. Nakutana na watu wa aina mbalimbali. Inawezekana mimi nawajua wengi wanaoteseka lakini sipingi kama wewe utakuwa umeshuhudia idadi kubwa zaidi yangu. Hebu tugawane elimu ndogo niliyojifunza mtaani.
Kuna pointi ambazo nitazieleza lakini kabla yake lazima nifafanue kuwa inawezekana ukawa unapata wapenzi wengi. Ukifumba macho na kufumbua wapo wamejaa. Hata hivyo, wanabaki kuwa watu wa kujifunzia mapenzi kwako.
Wanakuacha unaendelea kuzeeka nyumbani. Matokeo yake vijana wanakuona mzee, kwa hiyo kimbilio lako linakuwa ni kujifariji kwa waume za watu. Unaiba mwanaume wa mwanamke mwenzako.
Kutokana na kukata tamaa ya kuolewa, unakata shauri la kuzaa kabla ya ndoa. Huna wa kuzaa naye, kwa hiyo huyo mume wa mtu ambaye unatoka naye ndiye unabeba mimba yake. Kosa lako linamgharimu mtoto kuwa na baba wa kuiba.
Ni wa kuiba kwa sababu wenye baba yao halali wapo nyumbani, akitoka wanajua amekwenda kazini na atarudi jioni, mtoto wako yeye anamuona kwa msimu. Wakati mwingine akija unamwambia amwite ‘Anko’, ni kosa kubwa.
Je, ingekuwa ni wewe, ungefurahi kuambiwa umwite baba yako mzazi Anko? Kama utajisikia vibaya ni kwa nini umfanyie hivyo mwanao? Unayo nafasi ya kumtafutia baba yake halali, tena aliyetokana na ndoa inayokubalika.
NINI SABABU YA WATU KUCHENGWA NA NDOA?
Zipo sababu nyingi ambazo nitaziweka kwenye makundi ambayo itakuwa rahisi kuyaelewa. Katika kila kundi, nitaeleza tiba ambayo kama mtu atajiona linamhusu, basi akiitumia inaweza kumsaidia na atapata mwenzi wake wa maisha.
KUNDI LA KWANZA
Kuna aina ya watu ambao ni rahisi kuwaita vimbelembele ili kueleweka kwa wepesi zaidi. Ni mwanamke lakini anaamini ana nguvu nyingi kuliko mwanaume. Hajui kushuka chini daima yeye ni mtu wa kupanda juu.
Ni mwanamke lakini anataka awe na sauti yenye mamlaka na kumkoromea mwenzi wake anavyotaka. Akikaa na marafiki zake, anazungumza namna anavyoweza kukabiliana na wanaume kwa ubavu na kuwamudu. Anadhani sifa kumbe anaharibu sifa yake.
Itaendelea wiki ijayo.
www.globalpulishers.info
No comments:
Post a Comment