Mh,Balozi Mwanaidi Maajar akisisitiza jambo alipokuwa akiongea na Bloggers wa DMV akiwaelezea kuhusu matayarisho ya Miaka 50 ya Uhuru na mkutano wa DICOTA na kuwaomba BLOGGERS wote Marekani wasaidie kusambaza habari za sherehe hizi za Uhuru na mkutano wa DICOTA zitakazofanyika Sep 22-25,2011 Marriott Hotel iliyopo DULLES AIRPORT pia maeomba Watanzania wote Marekani wajiandikishe kwa wingi na anaomba kama inawezekana uchukue likizo mapema kusudi uwepo Washington,DC kuanzia alhamisi ya Sep 22,2011,kwani Miaka 50 ya Uhuru si kitu kidogo
Afisa Ubalozi Suleiman Saleh akichangia katika mkutano huo wa Bloggers wa DMV
Kulia ni Blogger Mubelwa Bandio(www.changamotoyetu.blogspot.com) akiwa makini kumsikiliza Mh.Balozi Mwanaidi Maajar na shoto ni afisa Ubalozi,Suleiman Saleh.
Blogger Sunday Shomari(www.sundayshomari.com)akifurahia majibu mazuri kutoka kwa Mh.Balozi Mwanaidi Maajar(hayupo pichani) baada ya kumuuliza swali.
Mh.Balozi Mwanaidi Maajar(wa pili kutoka shoto) akiongea na Blogger DMV,wa pili toka kulia ni afisa Ubalozi Suleiman Saleh,shoto ni Sunday Shomari na kulia ni Mubelwa Bandio
No comments:
Post a Comment