TANGAZO MAALUMU JUMUIYA YA WATANZANIA
Ndugu Wanajumuiya,Kama tulivyo wafahamisha hapo awali kuwa kazi mliyo tutuma imekamilishwa. Tuna washukuruni wote mlio leta na kutuma mapendekezo yenu kutokea mwanzo mpaka mwisho wa ukamilishaji wa Katiba mpya. Maoni yenu yote yalipokelewa na kufanyiwa kazi ndani ya Katiba, tunashukuru sana kwa mchango na muda wenu mliojitolea kwa nia ya kujenga Jumuiya yetu ya Watanzania.Hivyo basi, imetufikisha katika hatua kubwa na ya mwisho ya kuindeleza mbele Jumuiya yetu. Nakama tunavyo jua kuwa kwasasa hivi hatuna Jumuiya ila tuna Jina la Jumuiya na kwa sasa hivi Jumuiya haina Fedha za kujiendesha/ kuendesha shughuli zake. Kutokana na hali hiyo na muda wenyewe ulivyo pita, Wanakamati ya kuunda katiba tumependekeza kama ifuatavyo- Tutakuwa na Mkutano mkuu mmoja ambao utashughulikia maswala makuu mawili:
1. Shughuli ya kwanza itakuwa ya kupitia na kupitisha Katiba.
2. Shughuli ya pili itakuwa ya uchaguzi mkuu, tutachagua viongozi wa Jumuiya.
Hivyo basi tunaambatanisha na fomu ya uchaguzi.Kwa wale wote watakao penda kujitolea kugombea uongozi mbalimbali, tafadhali soma vizuri maelezo ya fomu hiyo na maelezo hayo yafuatwe kama yanavyosemwa. Hii itatusaidia kurahisisha kupata uongozi bora.Kila mgombeaji atakuwa na wiki mbili za kujaza/kushughulikia na kutuma fomu hizo. Wiki inaanzia tarehe 08/18/2011 – 09/01/2011. Na fomu hizo zitumwe na zikiwa na anuani zilikotoka na juu ya bahasha ziseme JUMUIYA YA WATANZANIA4023 APPLE JACK CTPASADENA, MD 21122Mwisho, Mkutano Mkuu utafanyika tarehe 09/17/2011 saa 4 asubuhi ( 10:00am). Anuani ya ukumbi wa mkutano mtafahamishwa hapo baadaye.
kwa form ya uchaguzi Bofya read more
KAMATI MAALUMU YA UCHAGUZI
2011
FOMU YA KUWANIA UONGOZI WA JUMUIYA YA WATANZANIA -WASH-METRO
WEKA VEMA KWENYE KISANDUKU / VISANDUKU KWA NAFASI UNAZOTAKA KUGOMBEA
[ ] RAIS WA JUMUIYA [ ] MWEKA HAZINA WA JUMUIYA
[ ] MAKAMU RAIS WA JUMUIYA
[ ] KATIBU MKUU WA JUMUIYA [ ] MJUMBE WA BODI YA JUMUIYA
Jina:________________________________________________________Jina la Ukoo:______________________________
(Tafadhali ambatanisha picha moja ya Pasipoti kwenye fomu hii, La sivyo maombi yako hayatafikiriwa)
Anwani ya mahali unapoishi:_____________________________________________________________________________
Tarehe ya kuzaliwa:_________________________________________Mahali ulipozaliwa___________________________
Simu ya nyumbani___________________________________________Simu ya kazini______________________________
Anwani ya Mtandao (E-mail):_________________________________ Simu ya mkononi____________________________
______________________________________________________________________________________
WADHAMINI:
Waombaji wanao wania nafasi hizi za uongozi wanatakiwa kupata wadhamini watatu (3) ambao ni Watanzania..
Wadhamini hao waweke sahihi zao kwenye nafasi iliyoonyeshwa hapa chini, La sivyo maombi yako hayatafikiriwa.
1. Jina:______________________________________________________________Namba ya Simu_______________________
Anwani ya Nyumbani:____________________________________________________________________________________
2. Jina:______________________________________________________________Namba ya Simu________________________
Anwani ya Nyumbani:____________________________________________________________________________________
3. Jina:______________________________________________________________Namba ya Simu_______________________
Anwani ya Nyumbani:____________________________________________________________________________________
ATC-ATC-ATC-ATC-ATC-ATC – ATC –ATC- ATC – ATC- ATC- ATC- ATC
SIFA ZA WAGOMBEA WA NAFASI ZOTE KATIKA JUMUIYA:
- Mgombea LAZIMA awe mtu mwenye sifa nzuri kwenye Jumuiya, awe na moyo wa uongozi na mtu asiyependa majungu, na pia awe na nafasi ya muda wa kujitolea bila kipingamizi cha kazi, maslahi, usafiri, nk.
- Mgombea LAZIMA awe na sifa za uongozi, atakayefuata Katiba ya Jumuiya, mwenye uwezo wa kubuni mipango na utekelezaji wake, mwenye msimamo bora usioingiliwa na vikundi au makundi, ili kuiongoza Jumuiya kwenye Malengo na Matarajio ya wanachama wake.
- Mgombea LAZIMA awe Mtanzania kwa kuzaliwa
Sahihi ya Mgombea___________________________________________Tarehe:_________________________________
Peleka FOMU hii pamoja na viambatanisho vyote kabla ya tarehe 1 September 2011 (MWISHO WA KUPOKEA MAOMBI) KWA ANWANI HII:
JUMUIYA YA WATANZANIA, 4023 APPLE JACK CT, PASADENA, MD 21122
2 comments:
Naomba kuuliza umri natumani ni miaka 18 na kuendelea,sawa je Mtanzania aliezaliwa hapa hastahili au nimeelewa vibaya?
Kuna sifa mbili muhimu hapa hazipo
Uzoefu ----- Awe na uzoefu wa kuongoza jumuia Fulani na kuifanikisha hususan awe anaweza ku-raise funds kwa ubunifu
Elimu ------- angalau awe amehitimu chuo kikuu
Makaratasi ----- awe na makaratasi sio chubwi
Post a Comment