Joyce Joliga,Songea
MKAZI mmoja wa Kijiji cha Lingusenguse, wilayani Namtumbo, Ruvuma, ameuawa kwa kuchomwa mkuki wenye sumu mgongoni wakati akiwa katika jarbio la kuiba nguo.Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Michael Kamuhanda, alisema, tukio hilo lilitokea juzi alfajiri, katika eneo la nyumba ya mkazi mmoja wa kijiji hicho.
Kwa mujibu wa Kamundaha, marehemu ametambuliwa kuwa ni Bashiri Mbunda na aliuawa baada ya kuzingirwa na wananchi, baada ya kuiba nguo mbalimbali.Kamuhanda aliwataka wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwa kuwaua watuhumiwa na badala yake, wawafikishe katika vyombo vya sheria

Habari nyingine zilisema polisi katika Wilaya ya Mbinga, mkoani Ruvuma, wanamshikilia mkazi mmoja wa Kijiji cha Mbangamawe, kwa tuhuma za kumiliki risasi tano, isivyo halali.Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Michael Kamuhanda, alisema mtuhumiwa alikamatwa juzi usiku, akiwa nyumbani kwake.
Alisema kukamatwa kwa mtu huyo, kulikuja baada ya raia wema kutoa taarifa polisi kuhusu kumiliki risasi hizo zinazotumika katika bunduki aina ya SMG.
"Baada ya taarifa hizo polisi walikwenda katika eneo la nyumba ya mtuhumiwa na kuweka mtego wa kumkamata, lakini alishituka na baadaye kukimbia. Hata hivyo polisi waliweka tena mtego mwingine na kufanikiwa kumkamata," alisema Kamuhanda.
No comments:
Post a Comment