Mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Michezo wa Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Leonard Tadeo akikabidhi kombe la ushindi kwa Nahodha Madina Iddi,mara baada ya kuibuka washindi katika mashindano ya Gofu ya wanawake kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati,ambapo Tanzania waliibuka Washindi.Michuano hiyo ya Chalenji ya gofu kwa wanawake iliyoshirikisha mataifa manne Kenya, Uganda, Zambia na wenyeji Tanzania, ilifunguliwa mnamo Agosti 16 kwenye viwanja vya Lugalo jijini Dar na kufikia tamati jana,Agosti 18
Mfunguzi wa Michuano hiyo ya Chalenji ya gofu kwa wanawake iliyokuwa ikishirikisha Mataifa manne Kenya, Uganda, Zambia na wenyeji Tanzania,Mkuu wa Majeshi mstaafu wa Tanzania, Jenerali George Waitara akimkabidhi trofi Nahodha wa Timu ya Gofu Wanawake Tanzania,Madina Iddi
Timu ya Gofu Wanawake Tanzania wakiwa na baadhi ya Wadau wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa kombe lao,kwa ushindi wao mnono walioiubuka nao kwenye michuano yaChalenji ya gofu kwa wanawake iliyoshirikisha mataifa manne Kenya, Uganda, Zambia na wenyeji Tanzania iliyofunguliwa mnamo Agosti 16 kwenye viwanja vya Lugalo jijini Dar na kufikia tamati jana,Agosti 18.
Baada ya kukabidhiwa kombe kwa timu ya Tanzania,ilikuwa ni furaha na vifijo kwa wadau wa mchezo huo
Timu ya Gofu ya Wanawake Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi Wadau
Mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Michezo wa Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Leonard Tadeo akiwavalisha medali wachezaji wa timu ya gofu Wanawake Tanzania.
Timu ya gofu Wanawake Uganda nao wakikabidhiwa zawadi zao pamoja na Medali,ambao waliibuka washindi wa nne katika michuano hiyo.
Mdhamini mkuu wa Michuano hiyo ya Chalenji ya gofu kwa wanawake iliyokuwa ikihirikisha mataifa manne Kenya, Uganda, Zambia na wenyeji Tanzania,Monica Ntege akiwavalisha medali wachezaji wa timu ya gofu Wanawake ya Zambia kwa kuibuka washindi wa pili katika michuano hiyo iliyofikia tamati jana,Agosti 18 katika viwanja vya Lugalo,jijini Dar.
Rais wa Chama cha Gofu cha Wanawake Tanzania (TLGU), Mbonile Burton akiwakabidhi zawadi wachezaji wa timu ya Gofu Wanawake ya Kenya,ambao waliibuka washindi watatu katika michuano hiyo.
Timu ya gofu Wanawake Tanzania,Wakishangilia mara baada ya kuvalishwa medali zao.
Menaja wa kinywaji cha Ndovu Specila Malt,kutoka TBL,Pamela Kikuli akiwa katika ya pamoja na baadhi ya wachezaji wa timu ya Gofu Wanawake Tanzania,pichani kulia ni Hawa Wanyeche,na watatu kulia ni Nahodha wa timu hiyo Madina Iddi pamoja na Angel Eaton.
Rais wa Chama cha Gofu cha Wanawake Zambia,Moono Mwila pichani kushoto akimkabidhi zawadi ya bendera ya chama chakeRais wa Chama cha Gofu cha Wanawake Uganda Dr Rose Azuba kuonyesha ushirikiano mzuri kwenye michezo.
Rais wa Chama cha Gofu cha Wanawake Tanzania (TLGU), Mbonile Burton akizungumza machache mbele ya mgeni rasmi pamoja na wageni mbalimbali waliofika kwenye tamati ya michuano hiyo,kwenye viwanja vya Gofu,Lugalo jijini Dar.
Wageni waalikwa mbalimbali walifika kushuhudia tukio hilo .
Timu ya Gofu Wanawake Tanzania wakishangilia jambo.Timu hiyo imeibuka kinara kwenye michuano yaChalenji ya gofu kwa wanawake iliyoshirikisha mataifa manne Kenya, Uganda, Zambia na wenyeji Tanzania iliyofunguliwa mnamo Agosti 16 kwenye viwanja vya Lugalo jijini Dar na kufikia tamati jana,Agosti 18.
No comments:
Post a Comment