ANGALIA LIVE NEWS

Monday, August 22, 2011

UBALOZI 1-1 WAZEE DC,MECHI YA DICOTA SUMMER EVENT

 Timu ya Ubalozi ikikaguliwa na Mh.Balozi
Timu ya Wazee DC ikikaguliwa na Mh.Balozi

Mechi kati ya Ubalozi na Wazee DC,timu ambazo zilikua zikitambiana takribani wiki nzima,jana zilishindwa kuibuka na ushindi baada ya kutoka suhuhu ya bao 1-1.

Sura nyingi mpya katika medani hii ya soka ukanda huu wa DMV zilionekana kwa mara ya kwanza zikisukuma gozi la ng'ombe kwa ustadi mkubwa na kuthibitisha usemi wa "MPIRA NI KAMA BAISKELI" hii ilionyesha jinsi gani DMV ina wachezaji wengi wenye vipaji.

Wachezaji ambao walikua kivutio ni Timu Kepteni wa timu zote Colonel Maganga wa Ubalozi na Mzee Muganda wa Wazee DC,wachezaji wengine ni Mayor Mlima,Eliud Mbowe,Sunday Shomari wa Timu Ubalozi,na Timu Wazee DC ni Abou Sakapala,Said Mwamende na golikipa Mobali Matinyi aliyekua nyota ya mchezo,kama asingekua yeye Wazee DC wangekula mvua ya magoli.

Mpira ulianza kwa Timu ya Ubalozi kulishambulia goli la wapinzani kwa mashabulizi makali muda mwingi wa kipindi cha kwanza Wazee DC walichezewa nusu uwanja,huko ngome ya Ubalozi ikiongozwa na Evans Shangarai akisaidiwa na Mashaka Bilal ikiwa likizo muda wote,mpaka kipindi cha kwanza kumalizika mabao yalikua 0-0.

Kipindi cha pili Wazee DC waliingia na sura mpya ya kitabu wakifanya mashambulizi ya kushutukiza wakitumia mwanya wa wapizani wao wanaposhambilia wao wanaagiza majalo na kunako dak ya 70 golikipa wa Ubalozi alijifunga mwenyewe baada ya kuudharau mpira uliopigwa kutoka wingi ya kulia na Luka kinyang'anyiro na kipa alipojaribu kuudaka kwa mbwembwe ukangonga mguu wake wa kulia na kuhesabu goli  la kwanza kwa Wazee DC.

Haikuwachukua muda kwa timu ya Ubalozi kusawazisha bao kupitia mchezaji wao hatari,Rodney Maganga aliyepokea pasi kutoka kwa Colonel Maganga aliyekua akicheza wingi ya kushoto na kutoa krosi kama David Beckham wa enzi hizo za Man U na mpira kumkuta mfungaji aliyepiga shuki hafifu na kumshinda kipa wa Wazee DC,Mobali Matinyi na huku beki ya Wazee ikijaribu kuuokoa lakini Refa Lemi Mhando alisema mpira uishavuka msitari na hivyo Ubalozi kusawazisha bao.

Baada ya kupata bao la kusawazisha timu ya Ubalozi iliendelea kulisakama goli la Wazee DC kama mbogo aliyejeruhiwa huku ikishangiliwa na Mh.Balozi Maajar,Mama Munanka,Mama Love Maganga na Wafanyakazi wengine wa Ubalozi lakini mpaka kipenga cha mwisho bao ni 1-1

No comments: