Advertisements

Sunday, August 21, 2011

VIJIMAMBO KIUNGO MUHIMU NDANI YA DMV!


Mpwa,
Napenda kukupa pongezi kwa kujitolea kwako kutupasha habari mbalimbali wakazi wa DMV. Inaeleweka wazi kazi ya uandishi wa habari ni ngumu na yenye miiko mingi kiutekelezaji. Vijimamambo imekuwa mstari wa mbele kutupasha habari bila ushabiki wa aina yeyote ile. Hii ni ngumu sana na umekuwa ukitekeleza majukumu yako bila ya kuwa na hisia  zozote zile za uchochezi ndani ya jamii yetu. Vijimamambo si tu imekuwa kiungo cha habari ndani DMV bali imekuwa ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku.
Kwa kumalizia tu wakazi wa DMV tuendelee kumpa support Dj Luke; wote tunaelewa wazi umuhimu wa vijimambo ndani ya DMV
Ubarikiwe
Said.
----------------------------------------------------------------------------------
Said nashukuru sana mkuu lakini nataka kusema kwa kwamba shukrani za dhati zituendee sisi Watanzania kwa upendo,mshikamano,ukarimu na kufarijiana kwa kila siku iwe furaha iwe huzuni sote ni kitu kimoja na Utanzania ndio udugu wetu.
kwa maana hiyo,shukrani za pekee ziwaendee Watanzania wote DMV na Marekani kwa ujumla kwa kushikamana kuliko tukuka.


Na namuomba Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema azidi kujujalia,atupe nguvu,atujalie hekima tuweze kutambua mazuri na mabaya,atuepushe na majaribu,upendo wetu uwe wa kweli,daima tuwe kitu kimoja bila kujali udini wetu na mwisho tuwe mfano wa kuigwa na mataifa mengine.

Mungu Ibariki Afrika,Mungu Ibariki Tanzania na Watu wake.

2 comments:

Anonymous said...

ni kweli Luka unastahili hongera, keep it up !!

Anonymous said...

keep it Luke Joe!!!!!!