ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, September 3, 2011

Mapigano yaibuka mpakani mwa Sudan mpya-BBC

Mapigano yameibuka katika jimbo la Blue Nile nchini Sudan baina ya jeshi na majeshi yanayomtii gavana Malik Agar.
Bw Agar ni mkuu wa upinzani wa chama cha SPLM-Kaskazini na aliyekuwa kamanda wa waasi aliyeshiriki katika kufanikisha kupata uhuru wa Sudan kusini mwezi Julai.
Chama chake kimesema askari wa Khartoum walishambulia makazi rasmi ya Bw Agar na maeneo mengine kwenye mji mkuu, Damazin.
Huu ni mpaka wa tatu kushuhudia mapigano tangu uhuru wa Sudan kusini.
Na katika eneo jirani la Kordofan kusini, serikali imekana kuhusika na mashtaka ya mauaji ya kimbari baada ya takriban watu 200,000 kukimbia makazi yao.
Siku ya Jumanne, serikali ya Sudan iliwasilisha malalamiko kwa baraza la usalama la umoja wa mataifa, ikiishutumu Sudan kusini kwa kuwaunga mkono waasi wa Kordofan kusini.
Pia kumekuwa na mapigano Abyei, eneo linalozozaniwa na pande zote mbili.
Mwandishi wa BBC James Copnall mjini Juba amesema haya ni mapigano ya mwanzo kuibuka huko Blue Nile tangu ghasia za baina ya kaskazini na kusini kumalizika mwaka 2005.
Lakini alisema eneo hilo wakati wote lilikuwa kwenye hatari kutokana na kupakana na Sudan kusini na imegawanyika baina ya wanayoiunga mkono serikali ya Rais Oma al-Bashir na kundi la SPLM.
Jeshi la Sudan limesema majeshi yake yalishambuliwa na yale ya Bw Agar.

No comments: