Saturday, September 3, 2011

MECHI YA WAZEE NA VIJANA JUMAPILI SEP 4,2011,Meadowbrook pk,Maryland


KESHO,Jumapili ya Sept 4,2011 kutakua na Mechi ya kukata na shoka kati ya timu ya Wazee na Vijana kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya IDD .

Mechi hii imeandaliwa maalum kati Kocha mchezaji wa DC Nyalugusu,Jabir Jongo na Timu Kepteni wa Bango Real FC,Ally Bambino,mechi hii imetabiriwa kuwa ya upinzani mkali kwani ni mechi kama DC Nyalugusu na Bongo Real FC isipokua ni majina tu yamebabilika.Kitu kingine katika mpambano huu ni mchanganyiko wa wachezaji kwani Timu Kepteni wa Bongo Real,Ally Bambino na Kocha mchezaji wa DC Nyalugusu watachezea timu moja kwa maana kwamba mechi itakua ngumu na ya kusisimua

Kawaida DC Nyalugusu ndio timu inayokuwa na wachezaji Vijana wengi na Bongo Real FC ni timu ya Wazee,Wakiulizwa Jabir Jongo na Ally Bambino wao walisema hizi timu ni moja tunapotumia majina ya DC Nyalugusu na Bongo Real hua tunajaribu kuongeza ukali wa mechi na tunapotumia Vijana na Wazee tunapinguza ukali wa mechi na kama unavyojua watu wametoka kwenye Saumu kali,Wachezaji wanahitaji mechi nyepesi.

Mechi hii itakua nzuri kwani itakua na Udc Nyalugusu na Ubongo Real ndani yake,tu naomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kwani hii itakua kama IDD pili kwa huku kwetu na kipute kinatarajia kuanza saa 10:30 Jioni(4:30pm)

Mechi inatarajiwa kuanza mapema kwani jua limeishaanza kuzama mapema.tunaomba wachezaji wote wakipata ujumbe huu wawataarifu wengine.

No comments: