NAAM kama ilivyo ada yetu tumekutana tena kwenye kona yetu. Nina imani kila mmoja hajambo pia nawapa pole wote waliokutwa na mashkili, nawaombea kwa Mungu wamalize matatizo yao.
Bila kupoteza muda ningependa nianze mara moja mada yetu ihusuyo thamani ya ndoa. Ningependa kwanza tujiulize ndoa ni nini?
Ndoa ni baraka za uhalalisho wa watu wawili wenye jinsia tofauti kuishi pamoja. Pia ni muunganiko wa halali wa mwanamke na mwanaume kuwa mwili mmoja. Nina imani mpaka hapo utakuwa umenielewa vizuri zaidi.
Bila kupoteza muda ningependa nianze mara moja mada yetu ihusuyo thamani ya ndoa. Ningependa kwanza tujiulize ndoa ni nini?
Ndoa ni baraka za uhalalisho wa watu wawili wenye jinsia tofauti kuishi pamoja. Pia ni muunganiko wa halali wa mwanamke na mwanaume kuwa mwili mmoja. Nina imani mpaka hapo utakuwa umenielewa vizuri zaidi.
Je, nini thamani ya ndoa kwa mwanadamu?
Ni kujitoa katika vitendo vya kuzini yaani kufanya mapenzi pasipo baraka toka kwa Mungu. Ndoa hujenga heshima ya mtu na kumwekea mipaka ya utaratibu wa maisha ambayo humpendeza Mungu.
Nini hasa nia na madhumuni ya mada hii?
Ni kutokana na utamaduni wa sasa watu kushindwa kuheshimu ndoa zao kwa kufanya mambo ambayo hayamtofautishi mtu kabla na baada ya kuoa au kuolewa.
Tunashuhudia jinsi wanawake au wanaume wametawaliwa na tamaa za kimwili na kutoka nje ya nyumba zao na kuwaacha wenza wao kama fenicha ndani.
Tujiulize nini makusudio ya kuoa au kuolewa?
Ni kuanza maisha safi yampendezayo Mungu, pia kujenga familia nje ya wazazi wako. Mpaka unaamua kuoa lazima utakuwa umeridhika na mpenzi wako na kuwa tayari kuanza safari ya maisha pamoja.
Nini kinachotakiwa kufunga ndoa?
Kwa vile mmeamua kuwa mwili mmoja, basi ninyi huwa kama viungo vya mwili. Sidhani kuna kiungo kitamtegea au kumchukia mwenzake. Kikiumwa kidole basi mwili mzima utaumwa. Katika mapenzi vile vile ni kuwa kitu kimoja kwa taabu, raha na kuridhika na mwenzako.
Kwa mwanaume kumpenda mkewe na mwanamke kumheshimu mumewe. Wanandoa lao huwa moja, hukaa chini na kujadiliana pamoja kuondoa kero zinazoweza kuweka nyufa ndani mwao.
Kuoa ni kufunga mlango wa mabaya yote na kujenga pepo ya duniani. Wanandoa pendaneni mapenzi ya kweli yenye upendo na huruma. Mke asimuudhi mumewe vile vile na mumewe asifanye hivyo.
Ila kuna watu huingia kwenye ndoa kwa kufuata mkumbo hata hufanya jambo lolote lililo nje ya ndoa bila wasiwasi wasi.
Siyo waoga wana kiburi hawaridhiki na mpenzi mmoja, wametawaliwa na tamaa ya mwili zaidi kuliko upendo, si wakweli hutawaliwa na uongo, mambo yao mengi yametawaliwa na usiri zaidi.
Hawajutii makosa yao huamini wapo sahihi kwa kila walifanyalo, ndoa hizi hazidumu huvunjika wakati wowote au huwa mateso kwa upande mmoja. Aliyeingia katika ndoa kwa dhamira ya kweli ni mpole mnyenyekevu mwenye huruma.
Huchukia kila lililo baya, ni mwalimu mwema kwa mwenzake na kuwa mbunifu wa kuongeza furaha ndani ya nyumba yao. Ndoa hizi hujaa baraka na amani.
Thamani ya ndoa ni kubwa kuliko unavyofiria ndoa si maigizo bali kujitoa kwa ajili ya wenzako lazima mtafanikiwa.
Kwa hayo machache tukuane wiki ijayo.
www.globalpublishers.info
No comments:
Post a Comment