Kwa niaba ya Umoja wa Watanzania North Carolina (UTNC) na Jumuiya ya Wenyeviti wa Jumuiya za Watanzania Marekani (TCLA-USA)
Mimi pamoja na Watanzania wote wanaoishi Marekani tunaungana na ndugu,jamaa na marafiki wote duniani kwa maombolezi ya msiba mzito uliotokea Tanzania,Zanzibar. Taarifa za maafa zimetufikia kwa mshtuko mkubwa. Wengi wa jamaa na ndugu zetu wamepoteza vipenzi vyao, na wengi wapo katika hali ya majeruhi. Kwa karibu tumekuwa tukifatilia juu ya taarifa hizi za kuzama kwa meli. Hiki ni kipindi kugumu mno kwa watanzania walio wengi. Tushirikiane kwa pamoja,tusaidiane na kuombeana dua.
Kama taarifa mlizozipata kutoka kwenye vyombo vya habari, watu waliopoteza maisha yao ni wengi na majeruhi ni wengi. Hiki ni kipindi cha kushikamana, kuhurumiana na kusaidiana. Kipindi hiki ni kigumu pia kwa ndugu walio mbali na watu wao.
Mpigie simu ndugu yako unayehisi atakuwa yupo katika hali ngumu, nenda ukakae naye kwa maliwazo na kwa msaada unaohitajika. Hakikisha ndugu yako anapata bega la kuegemea. Msiba huu ni mzito, mungu atujaalie tuwe pamoja zaidi.
Kwa hakika msaada mkubwa unahitajika. Kila mmoja wetu ajitahidi kushiriki kwa upande wake kwa hali na mali kusaidia. Tuonyeshe umoja wetu na nguvu zetu katika shida na majaribio makubwa kama haya.Kuwa karibu na wafiwa, tenga muda kwa kukaa pamoja nao na kusaidiana.
Watanzania ni watu wenye upendo na huruma. Kila mtu ajitahidi kumpigia simu mwnziwe kumjulia hali na kumpasha habari na kujua zaidi. Huu ndio upendo wetu na utu wetu, uliojengwa kwa misingi ya utaifa wetu.
Watanzaniani watu ambao tunashirikiana kwa hali na mali, na ni watu ambao hatukubali kumuona mwenzetu anapata shida.
Mwenyezimungu awalaze mahala pema ndugu zetu waliotangulia. Awape ustahamilivu ndugu zetu wafiwa, awape nguvu ndugu zetu waliojeruhiwa na ajali hii. M/Mungu alipenguvu taifa letu la Tanzania katika kipindi kigumu hiki na kutuvusha salama.
Nassor Ally,Chairman
UTNC & TCLA
P.O.Box 52531
Durham,NC 27717
No comments:
Post a Comment