Mkutano mkubwa wa Neno la Mungu pamoja na tamasha la Uimbaji wa aina yake utafanyika hapa District of Columbia, Maryland na Virginia kuanzia Jumapili tarehe 2 hadi 9 October 2011 kuanzia saa 11jioni hadi saa 3usiku ( 5pm-9pm). Wahubiri Maarufu toka Tanzania, Askofu Peter Kitula na Mchungaji Grace Mbise wamealikwa na wataingia jijini tarehe 1 October 2011. Waimbaji Mashuhuri toka Tanzania, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro na Chistina Shusho nao wameaalikwa na wanaingia Washington DC kesho September 29 2011. Waumini mbalimbali toka Tanzania, Kenya na Uganda pia wamealikwa. Waleteni watu wote wenye shida mbalimbali za kimwili na Kiroho na wagonjwa wataombewa. Tegemea muujiza wako toka kwa Mungu katika siku hizo za mahubiri.
WOTE MNAKARIBISHWA

No comments:
Post a Comment