Tuesday, September 6, 2011

Tunaambiwa wanaume wenye mishipa ni ‘spesho’, tujifunze pamoja

WANASEMA kipendacho roho hula nyama mbichi. Inasisitizwa kuwa siyo kinachokuvutia wewe kinaweza kumkonga moyo mwenzako. Ndiyo maana yule anapenda wapenzi wafupi, mwingine kama siyo mrefu hang’oki.

Kuna uvumi niliamua kuufanyia kazi. Kwamba wanaume wenye mishipa a.k.a mizigo wako vizuri kimapenzi. Inabainishwa kuwa kuna wanawake wa ukanda wa Pwani hawataki sampuli nyingine. Wao mizuka yao ipo kwa watu aina hiyo.


Wiki iliyopita nilitembelea Bagamoyo, nikapita ukanda wa Barabara ya New Bagamoyo. Lengo ni kupata maoni, kwani huko ndiko kwenye sifa ya kuwapo kwa wanaume aina hiyo. Nilifanikiwa kuzungumza na watu kadhaa ambao walinijuza yafuatayo:

ZABIBU SHOMARI ‘MAMA FEDA’
 Ni mama mwenye umri wa miaka 46. Kama ilivyokwa usemi ukubwa dawa, alinifahamisha kwamba yeye amewahi kutoka na wanaume wawili wa sampuli hiyo kati ya miaka ya 1990 na mwanzoni mwa miaka ya 2000.

“Kuna joto ambalo wanalo, hilo ndilo lililovutia na kuwachanganya wengi. Tulipokaa kwenye vikao vya kusukana, tuliwazungumzia wao. Kila aliyebahatika kupata habari ya mwanaume wa aina hiyo, alizungumza kwa ufahari kama ilivyo kawaida ya soga.

“Hivi sasa wanaume wenye mishipa wanakwisha. Elimu imekuwa nyingi, kwa hiyo tunafahamu kuwa ni ugonjwa. Kipindi kile baadhi yetu tulidhani ni tunu ambayo mwanaume anakuwa amepewa ili kuzalisha raha zenye ujazo wa kipekee kwa mwanamke.

“Kipindi kile wanaume wengi walijulikana wana hali hiyo, kwa hiyo tulipoketi na waume zao tuliwauliza wanapata nini? Mwanamke naye hakutaka kubaki nyuma, kwa hiyo alimpamba mume wake kwa namna alivyoweza. Alimsifia kwa uhodari wake kila wanapokutana faragha.

“Kutokana na sifa hizo, kuna watu walisaliti ndoa zao ili kuona manjonjo ya ziada ya wanaume wa aina hiyo. Kwa wale wasiokuwa na ndoa, nao walijaribu. Baadhi yao walinogewa wakakubali kuolewa ndoa ya mtala. Ila mimi katika uzoefu wangu sikuona kitu kikubwa sana zaidi ya joto la ziada kwenye maeneo hatari.”

MOSHI BINTI MAULID
Ni bibi mwenye umri wa miaka 58. Anajulikana zaidi kwa jina la Bibi Moshi. Wengi huenda kwake kupata ushauri wa kimapenzi, kwa hiyo ni kungwi wa kizazi cha sasa na kati. Anasema: “Mimi nina uzoefu, kwani hata marehemu mume wangu alikuwa hivyo.

“Hata mwanaume niliyezaa naye mtoto wangu wa kwanza alikuwa hivyo. Bahati mbaya, wote kwa sasa ni marehemu (mtoto na baba). Kuna kitu kimoja ambacho naweza kukichambua kutokana na uzoefu nilioupata kwao pamoja na hadithi za watu wengine.

“Ni kwamba ule mzigo huwa unachochea hisia ambazo wengine hawana. Mtindo ambao unaweza kufanya hisia hizo zije ni ule ambao mwanamke analala mfano wa mende anayekufa. Hapo kweli mkong’oto unapatikana.

“Ukiachana na hilo, baada ya hapo ni kila mwanaume kuwa na uwezo wake wa kusafiri umbali mrefu au karibu. Kwa hiyo kiasi cha muda shughulini hutegemea na aina ya mtu mwenyewe. Kingine ambacho wanalingana ni uzito. Mara nyingi siyo wepesi.

“Kuna wengine hujitahidi kupambana, hujitahidi kuwa wepesi lakini kwa uzoefu nilionao ni kuwa kasi yao huwezi kuilinganisha na wanaume wasio na hali hiyo. Binafsi nashukuru elimu inayotolewa, imeweza kumaliza tatizo, kwani kuna kipindi ilitaka kuonekana ni fasheni wakati ni ugonjwa.”

FADHILI MIATANO
Umri miaka 53, anasema: “Nilikuwa na tatizo hilo, bahati nzuri nimepona baada ya kufanyiwa upasuaji. Wakati bado nina tatizo hilo, kuna wanawake walinitongoza ili nihusiane nao. Mwanzoni nilishangaa sana kutokana na hali niliyokuwa nayo lakini baadaye nilizoea.

“Niligundua kumbe kuna mambo fulani ambayo hawayapati kwingine. Mpaka wake za watu walinitongoza lakini tangu nimepona, sioni pirika za wanawake hao. Napenda kushauri kuwa ule ni ugonjwa, kwa hiyo siyo vema kujivunia kuwa na mwanaume wa aina hiyo kitandani.”

HITIMISHO
Ushauri wangu upo pale alipomalizia mzee wangu Miatano kuwa isichukuliwe kuwa na mshipa ni ufahari, bali ni ugonjwa. Kwa hiyo tusaidiane kumaliza tatizo. Nimeleta mada hii kutokana na maombi ya wasomaji wangu ambao nao walidai kusikia uvumi huu kwa muda mrefu.

www.globapublishers.info

1 comment:

Anonymous said...

Toba!