ANGALIA LIVE NEWS

Monday, October 24, 2011

UN FAMILY DAY YAFANA KATIKA VIWANJA VYA LEADER'S CLUB

Mwishoni mwa wiki kulifanyika UN Family Day katika viwanja vya Leaders Club wakati wa Shamrashamra za wiki ya maadhimidho ya 66 ya Umoja Mataifa nchini ambapo ilipigwa  mechi kati ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa (White Jersey) na wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (Blue Jersey) ambapo timu ya Wizara ya Mambo ya Nje iliibuka kidedea baada ya kuichapa timu ya UN bao 4-2.
Wazazi wakionekana kufurahi na watoto wao katika mkusanyiko huo uliokutanisha Familia za Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Kucheza pamoja, kula pamoja, kunywa pamoja na kushiriki michezo mbalimbali.
Familia zikiwa pamoja.
Mgeni rasmi Mkuu wa Itifaki Balozi A. Itatiro akizungumza machache wakati wa UN Family Day na kusema kwamba siku hiyo haikuwa ya kusoma risala bali ni siku ya kufurahi pamoja....Happy Birthday UN..!!!
Kwa picha zaidi Bofya Hapa

No comments: