ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, November 3, 2011

HAPA NA PALE KATIKA PICHA

Waziri wa Maliasili na Utalii Bw. Ezekiel Maige (wapili kushoto), akiangalia moja ya Bunduki zinazoruhusiwa kwa ajili ya uwindaji wanyamapori, aliposhiriki kwenye mahafali ya 46, mkoani Kilimanjaro juzi. Wapili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi Chuo cha Uhifadhi Mweka, Profesa  Feetham Banyikwa. (Picha na Tulizo Kilaga)
Mtaalam wa dawa asilia za magonjwa sugu Bw.Nyakiziba Nyakubaho akitoa maelezo kwa wananchi kuhusu dawa hizo, kwenye banda lake, wakati wa Maonesho ya Mwanamke Mjasiliamali (MOWE) yanayo Dar es Salaam. (Picha na Prona Mumwi)
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Dodoma, Bi. Felister Bura akitaka ufafanuzi wakati Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma ikipitia mahesabu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Kushoto ni Bi. Amina Mwidau Mbunge Viti Maalum mkoa wa Tanga. (Picha na Peter Mwenda)
Hawa ni wapiga debe wa Boti ziendazo Visiwani Zanzibar wakiwa wameizunguka Bajaj iliyobeba abiria ili kuwashawishi kusafiri kwa boti wanazoziwakilisha kama walivyokutwa na kamera yetu eneo la Bandari, Dar es Salaam jana. (Charles Lucas).

No comments: