.jpg)
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema kuwa viongozi ambao wanatibiwa nchini India hali zao ni nzuri na wanatarijia kurejea nchini mwezi huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Membe alisema ifikapo mwisho wa mwezi huu wote watakuwa wamerejea.
Alisema hali ya Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya; Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Cyril Chami; Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, zinaendelea vizuri.
Akizungumzia hali ya Zitto, alisema kuwa anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa operesheni juzi na viongozi wengine wataruhusiwa hivi karibuni kurudi nchini ili waendelee na majukumu yao.
Wakati huo huo, Membe alisema vita ambayo inaendelea nchini Somalia kati ya wanamgambo wa Al-Shaabab na majeshi ya Kenya na kusema kuwa anatarajia kushiriki katika mkutano ambao utafanyika Novemba 20, mwaka huu mjini Nairobi kujadili suala hilo.
Alisema atakutana na mawaziri wengine wa mambo ya nje kujadili jinsi ya kuisaidia nchi ya Kenya kupambana na kikundi hicho cha kigaidi na namna ya kuisaidia Somalia kukabiliana na na tatizo la njaa.
Membe alisema pia wataangalia matatizo ambayo wanayapata majeshi ya somalia pamoja na kuwasaidia nchi hiyo iweze kujilinda yenyewe pia watapatiwa mafunzo.
Alisema kuwa tatizo kubwa ambalo limeonekana ni kwamba huwa wanaenda katika eneo la bandari ambapo huwa wanaenda kununua vitu katika eneo hilo na hapo ndipo wanapofanyia uharamia.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment