ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, November 2, 2011

MSIBA MICHIGAN NA TANZANIA

Familia ya Marehemu mama Mgaye wa Tanga na Watanzania wote waishio Michigan wanasikitika kuwataarifu habari ya msiba wa Mtoto wao,Kaka,ndugu,rafiki mkubwa na Mtanzania mwenzetu Nassib Manyala uliotokea Jumamosi  Octoba 22, 2011 huko Lansing, Michigan.

Kwa sasa tunasubiri polisi kumaliza uchungunzi  na report kutoka kwa Medical Examiners.

Gharama za funeral home na kusafirisha mwili bado hazijajulikana na mara tupatapo report kutoka kwa vyombo husika tutawataarifu zaidi kwa sasa tunachoomba Watanzania tushikamane tuwe kitu kimoja tuwezeshe kumsafirisha mwenzetu Tanzania akapumzike kwenye nyumba yake ya milele.

2 comments:

Anonymous said...

JAMANI SI TULIAMBIWA KUNA BIMA YA DOLA MIA TATU? JAMANJ JAMANI. LUKA USIBANIE HII MAISHA NI MAGUMU SANA

Chebe said...

Ndugu said, ndio maisha ni magumu sana. Na kutokana na huo ugumu wa maisha ndio maana tunasidiana. Unafikiri hiyo dola mia tatu inatosha kweli? Kama unacho toa, kama huna basi wengine watasaidia walichonacho. Kumbuka leo kwako kesho kwa mwenzio. KUTOA NI MOYO