ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, November 3, 2011

OMBI LANGU, NI MCHANGO WA MAWAZO YENU

Kukiwa na shughuli mbalimbali naona moja ya perfomance ni KHANGA SHOW. Jamani Tanzania ina vitu vingi vya kitamaduni vya kuonyesha si tu mitindo ya uvaaji wa khanga tu.Zikiwemo show za khanga, bado vijana wanaweza  kuungana na kuanza kujifunza ngoma za makabila mbalimbali,  maigizo,majigambo,mashaili,nkonkoti,mapishi mbalimbali ya vyakula na kuweza kutumbuiza katika hafla mbalimbali za kitanzania.Taasisi zetu mbali mbali kama vile makanisa,vyama,jumuiya n.k anzisheni vitu hivi nasi tutasaidia.Bahati nzuri sasa tuna blog mbalimbali zinazomilikiwa na watanzania wenzetu ambazo zitasaidia kuvinadi vikundi hivi.
Kwa hapa marekani ndiko tuna nafasi kubwa ya kuonyesha utamaduni wetu zaidi kuliko nchi zingineko. 
Nawatakia mafanikio,
Projestus.

6 comments:

Anonymous said...

Habari Kaka, naona umeongea kuhusu Khanga n.k sasa hao wenye Kanga wameona hiyo ni moja ya kuwakilisha utamaduni wetu. Sasa wewe anzisha kitu kingine kinachoweza wakilisha utamaduni wetu, hao wameanza na Khanga, sasa wewe unataka kuja na nini? itakuwa vizuri kama utakuja na idea moja na kusema mimi nitafanya hivyi basi itakuwa ni vizuri sana. Nikutakie siku njema.

Anonymous said...

mpe ukweli wake huyu naona amelala tu anaota na kuanza kuandika khanga kiboko yako,ni kweli wewe anzisha hizongoma ,n'gon'goti,n.k utafanya biashara siyo usubiri waanzishe uende kusaidia nini sasa Ma winnie wanawake na maendeleo bwana tusonge mbeleeeeeeeeeee

Anonymous said...

Kaka mtoa hoja unataka kusema nini? mimi nilidhani wewe una mpango wa kuanzisha sasa unataka watu wengine waanze halafu usaidie, utasaidia nini? wewe anza na ngoma au ngojela halafu watu wanaweza kujiunga nawe, sasa naona unatoa wito kwa wengine kuanzisha hapo ndio nashindwa elewa point yako nini. Naungana na mdau hapo juu kuwa wa Khanga wenyewe waliona utamaduni wetu ni huo basi wakawakirisha na kwa kweli wamefanyikiwa kiasi kikubwa sasa wewe njoo na ya kwako, unapoanza kusema Makanisa, jumuiya zianzishe...hapo nashindwa kukuelewa njoo na kitu kimoja kama watu wa Khanga walifanya. Nichangia tu...

Anonymous said...

Kaka bado hupo, wewe kwa mipango yako, sasa kama walivyosema wadau hapo juu wewe anza yako, ukianza na wengine watafuata. Sasa unaposema watu waanze halafu wengine mtasaidia, kwani wewe ni nani? wewe anza kwanza wengine wafuate.

Anonymous said...

Kaka,naona wewe unachuki binafsi,hive nikuulize hupo kwenye kitengo gani hasa ambacho unaweza kusaidia watu?au ukawaita watt wakakusikiliza sanasana utajikweza tu,wewe anzisha hicho chako unachoona Kitaleta tofauti ,hap a bwana Kila mtu anafanya Kama mtanzania kwa kujisaidia yeye mwenyewe mbona wapo wengi tu,ushauri wangu muone peter ligatel ulete vitu chako ila angalia Kila mtu asije akaanza na chake.

Anonymous said...

aaaaah kaishiwa huyo,anahaha tu ovyo alichonacho yeye chenye maendeleo ni kipi?wewe waache hao wenye kanga waendelee bwana leta chako na wewe tuone usilete vya watu hapa.unataka kujulikana kwa nguvu