NAAM, kama kawaida tumekutana tena kuendelea na mada yetu ambayo nina imani mliisubiri kwa shauku kubwa. Nami leo sipotezi wakati, tunaendelea tulipoachia wiki iliyopita.
Unapomuona mwenzi wako ametoka nje ya ndoa kisha wewe kulipa kisasi kwa kutoka nje ya ndoa, kama nilivyosema ni kuongeza ufa kama siyo kuibomoa kabisa nyumba yote.
Kumbuka kwenda nje ya ndoa kwa ajili ya kulipa kisasi humkomoi mumeo au mkeo, bali ni kuongeza tatizo juu ya tatizo, ni sawa na kuuzima moto kwa mafuta ya taa.
Msimamo wako pekee ndiyo utakaoiokoa nyumba yako ikiyumba, kuongeza tundu kwenye ngalawa lazima mtazama wote.
Kuna penzi la kweli kati yenu?
NA ALLY MBETU
Ninavyojua penzi la kweli lipo ndani ya moyo, lazima mtaoneana huruma na kutokuwa tayari kuipa uchungu mioyo yenu.
Ndani la penzi la kweli mtu huwa hatoki nje, huridhika na mwenzie kwa kuwa ndiye chaguo la moyo wake.

Mhusika katika uhusiano huo hayupo tayari kulipiza kisasi kwa kuwa anajua penzi la kweli halina kisasi bali kinachotakiwa kufanyika ni kumrudisha mwenzake kwenye mstari. Wapo wanaoshangaa kumwona mwanaume amemfumania mkewe na kumsamehe.
Mfano ukimfumania mkeo utachukua uamuzi gani? Nina imani asilimia 99.9 watasema: “Nitamuacha kwa kuwa si mwaminifu.”
Swali kama hilo ukiuliza kwa upande wa pili wa shilingi kuwa mkeo akikufuma wewe utachukua hatua gani? Hili sitaki jibu kwa kuwa unalo mwenyewe.
Kinamama siku zote huwa wanyonge, hata wakifumania huishia kulia tu.Nia yangu si kutaka mshindane kufumaniana, la hasha.
Hakika wengi wetu tumekuwa si waaminifu ndani ya nyumba. Kwa sasa imekuwa fasheni kila mtu kuwa na watu wawili nje au zaidi.
Ukiuliza utaambiwa kaanza mwenyewe au kanisingizia kwa muda mrefu, sasa ninafanya kweli. Huo ni uongo, kila afanyae kitu amedhamiria kwa muda mrefu, alitafuta sababu tu ya kufanya uchafu wake.
Kama si tabia yako, nakataa katu, kwani mtu kukusingizia haikupunguzii kitu mpaka uamue kulipa kwa kufanya kweli. Mwenzio asilie wivu, kisa utafanya kweli? Utatembea na wangapi kwa kusingiziwa? Au mpenzio kutembea nje?
Uchunguzi wangu ambao nina uhakika nao ni kwamba, asilimia 100, tabia za kulipizana kisasi kwa kutoka nje ya ndoa kwa kisingizio cha “unafanya kweli”, zinafanywa na wale ambao wamekuwa na asili ya tabia hiyo ila walificha makucha.
Hapa kuna mambo mawili. Kati ya watu wawili hao, kuna mmoja ambaye moyo wake hubadilika na kuwa tayari kuwa na wewe kwa shida na raha. Lakini mmoja huwa habadiliki, huu huwa mwanzo wa mateso ya mmoja.
Kwa kuwa ulikuwa hujauandaa moyo wako japo ulikubali kuwa na mwenzio, tatizo lolote linapotokea ni upesi kulipa kisasi, watu hawa siku zote hutaka mwende sawa, ukimzidi hakubali na yeye atalipiza ili muwe sawa.
Wajua nini hasara za kulipa kisasi cha mapenzi?
Tukutane wiki ijayo kwa muendelezo wa mada hii.
www.globalpublishers.info
No comments:
Post a Comment