Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila
BAADA ya Chama cha NCCR-Mageuzi kumfukuza uanachama mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila sasa kinasuasua kulijulisha Bunge kwa barua kuwa mbunge huyo kijana siyo mwanachama wa chama hicho.
Mwananchi pia limebaini kwamba, Kafulila pamoja na wenzake bado hawajakabidhiwa barua za kufukuzwa kwao na Hlmashauri Kuu (Nec) ya chama hicho, uamuzi ambao umepata upinzani mkubwa kutoka kwa watu na taasisi mbalimbali nchini.
Jana viongozi wa NCCR Mageuzi walipoulizwa walitupiana mpira kuzungumzia suala hilo, ikiwa ni wiki moja tangu Nec ya chama hicho kumvua uanachama Kafulila kutokana na kile kilichodaiwa ni kosa la kuzungumza siri za ndani za chama katika vyombo vya habari.

Kafulila alifukuzwa uanachama pamoja na wenzake watatu, akiwemo aliyekuwa mgombea urais wa chama hicho katika uchaguzi wa mwaka jana, Hashim Rungwe. Katibu Mkuu wa chama hicho Samwel Ruhuza alisema huenda barua hiyo ilipelekwa katika ofisi za Bunge jana huku akishikwa na kigugumizi kufafanua zaidi na kuomba atafutwe Mkuu wa Idara ya Oganaizesheni, Kampeni na Uchaguzi wa chama hicho, Faustine Sungura. “Sijui wameshapeleka…, itakuwa wamepeleka bungeni, inawezekana ikawa wamepeleka leo (jana), ila sitaki kufafanua zaidi wala ku ‘confirm’ (kuthibitisha) kwa sababu nipo safarini,” alisema Ruhuza.
Hata hivyo, gazeti hili lilipomtafuta Sungura alisema hafahamu chochote kuhusu suala hilo huku akimrushia mpira Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, George Kahangwa. Kahangwa alipoulizwa alisema hawezi kujibu lolote na kutaka iulizwe ofisi ya bunge. “Iulizeni ofisi ya bunge kama barua hiyo wameshaipata ama laa…, unajua hatupendi kuzungumza masuala haya tena, hivi sasa mkitaka maelezo waulizeni wahusika wenyewe, kama chama tumeshafanya kikao na kutoa uamuzi,” alisema Kahangwa.
Alipoelezwa kwamba yeye ndio ana majibu ya taratibu zinazofanywa na chama hicho kulijulisha bunge juu ya barua hiyo, aliendelea kusisitiza kwamba huo ndio uamuzi wa chama.
Waliotimuliwa hawajapewa barua Habari zaidi zinaeleza Rungwe, Kamishna wa mkoa wa Tanga Mbwana Hassan na Yotham Rubungira wa Mwanza ambao walitimuliwa uanachama pamoja na Kafulila nao bado hawajapewa barua zao za kufutwa uanachama. Akizungumza kwa njia ya simu jana, Rungwe alisema mpaka sasa hajapewa barua yoyote ya kuvuliwa uanachama,” Mpaka sasa sijapewa barua yoyote ndugu yangu, hakuna barua kimya kabisa.”
Lakini, akifafanua suala hilo Kahangwa aliendelea kusisitiza kwamba watafutwe wahusika wenyewe ili waweze kujibu kama wameshapewa barua hizo. Juzi Mwananchi lilimshuhudia Rungwe na Ruhuza wakishiriki katika moja ya vikao vilivyoandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), kilichofanyika katika hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.
Haikuweza kufahamika mara moja madhumuni ya kikao hicho ambacho pia kilihudhuriwa na Mwenyekiti wa United Democratic Party (UDP), John Cheyo. Katibu wa Bunge Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari (siyo Mwananchi) akisema uamuzi wa Nec ya NCCR Mageuzi dhidi ya Kafulila, utakubaliwa na Bunge iwapo demokrasia katika kuufikia itakuwa ilizingatiwa.

“Inategemea watakavyotuandikia. Si unakumbuka mwaka ule NCCR walivyopeleka kwa Spika taarifa za kuwavua uanachama Marando na Chiku Abwao, lakini Spika akakataa kutokana na kikao kilichowavua kuwa na matatizo? Sasa kikao kitaangaliwa, pia sababu zitaangaliwa. Kwa sababu hii ni nchi ya demokrasia. Hivyo, lazima demokrasia iangaliwe,” alisema Dk Kashililah.
Tendwa Kwa upande wake Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, John Tendwa alionyesha dhahiri kumkingia kifua Kafulila huku wakikitaka NCCR kutafakari kwa kina uamuzi huo. Tendwa alivitaka vyama vya siasa kutumia busara katika kutatua migogoro yake na siyo kutoa uamuzi wa kukomoana kama wa kumfukuza mtu uanachama.
“Kila mara nasema kwamba, vyama viwe makini panapotokea migogoro. Wafanye majadiliano kupitia vikao na sio kuchukua uamuzi wa haraka kufukuzana uananchama,” alisema Tendwa na kuongeza:
"Kuandaa uchaguzi mdogo ni gharama kubwa. Uchaguzi mmoja gharama yake ni zaidi ya Sh19 bilioni. Kwa suala kama hili tujiulize nani amesababisha gharama, tusiishie tu kuupigia kelele ufisadi, tuangalie na sisi viongozi wa vyama tunaisaidia vipi serikali?”
Alisema alisema, Kafulila bado ana nafasi ya kukata rufaa ndani ya chama chake na hata nje ya chama. Alifafanua: “Ana uhuru kwenda mahakamani na akishinda ataendelea kuwa mbunge". Kafulila alivuliwa uanachama katika kikao cha dharura cha Nec kilichofanyika wiki iliyopita, kitendo ambacho kilimfanya kuangua kilio cha kwikwi kwa takriban dakika 40.
Mbunge huyo pia amekuwa akituhumiwa kuratibu mapinduzi dhidi ya mwenyekiti wa chama hicho taifa, James Mbatia kutokana na kile anachodai ni kukipotezea chama mvuto na kukifanya CCM B.
Hata hivyo, upepo wa kisiasa ulibadirika ghafla katika chumba cha mkutano wa Nec ambao badala ya kumng’oa Mbatia, Kafulila alijikuta aking’olewa kwa kura 38 huku 18 zikimngia kifua na nyingine, kuharibika.

Mwananchi
No comments:
Post a Comment