ANGALIA LIVE NEWS

Monday, December 12, 2011

Simu, mitandao ya kijamii, vinawatesa wengi - 2

AWALI ya yote, napenda shukurani zangu za kipekee nizielekeze kwa Muumba wa ardhi na mbingu kwa jinsi anavyonifanya niishi maisha ya staili hii. Ameamua kuniruzuku kwa kiasi hiki na kwa kudura zake, ataniongeza zaidi!

Tupo kwenye muktadha wetu unaosema: “Simu, mitandao ya kijamii, vinawatesa wengi .” Niliandika jinsi watu wanavyotengana au wanandoa kukosa suluhu kwa sababu ya simu. Namna baadhi yetu tunavyokosa uhuru na amani na kuishia kuwapiga marufuku wenzi wetu wasishike ‘viselula’ vyetu, tukihofia siri zetu kugundulika.


Na tatu ‘niliwabonda’ wale wataalamu wa ‘kusevu’ namba za wenzi wao wa pembeni kwa majina tofauti, wanaume kuandika ya kiume na wanawake kuweka ya kike. Haya ni mapenzi ya mashaka.
‘Ki ukweli’ simu za mkononi ni utandawazi uliojaa chembechembe nyingi za sumu katika uhusiano wa kimapenzi na hii imetokana na watu wengi, kukosa ustaarabu na kuzitumia kuwasaliti wenzao.

Hata hivyo, dhamira ya mada hii ni kukuandikia mbinu kadhaa zitakazokufanya wewe uishi na amani, bila kuzichukia simu kama dada yangu, Jasmin Mdanzi wa Nyakato, Mwanza ambaye sms yake niliiandika wiki iliyopita.
Pamoja na mbinu hizo, ningependa nikufahamishe kuwa haya nitakayoyaandika kama wewe utashindwa kuyafanyia kazi inavyotakiwa, hakuna kinachoweza kufanyika.

Mosi, wewe na mpenzi wako mnapaswa kuwa na uelewa mkubwa, kwa kutambua ukweli. Pili ni kuacha papara, mambo ya kusikia simu ya mpenzi wako inaita, unairukia na kutaka kujua anayepiga au aliyetuma ujumbe, vimepitwa na wakati.

ANGALIZO; Inawezekana akawa hana tabia ya kucheza mechi za nje, lakini wivu wako wa kupitiliza ndiyo unaomfanya ashindwe kuwa huru. Hata Zainab ambaye ni dada yake ofisini, anamuandika Zidane kwa ababu ukikuta jina la kike hauwezi kumuelewa hata akuambieje.

Hujawahi kuona, mtu anamuelewesha kuwa fulani ni dada yake ambaye hushirikiana kwa ukaribu ofisini, lakini mama nyumbani haelewi, hapo matokeo yake ni jamaa ‘kumsevu’ Ramla kama Ronaldo.

Pointi ni hizi zifuatazo, naamini ukizisoma kwa herufi katika kila mstari, utapata kile kitu ambacho binafsi nimekikusudia, pia utaweza kuondoa migogoro isiyo na ulazima.

KUJIAMINI!
Inawezekana wewe ni muaminifu katika mapenzi yako, lakini tabia yako ya kujishtukia mara kwa mara kila anapokuomba simu, inamfanya aanze kuwa na mashaka juu yako.
Anajiuliza, kwa nini haupendi ashike simu yako? Elewa kuwa jibu atakalolipata hapo ni kuwa kuna mchezo mchafu unaomchezea, na unaufanya kupitia simu ndiyo maana unailinda kama nguo ya ndani ambayo huivua wakati wa kuoga tu!

Tuweke kituo mtu wangu, naomba tukutane Jumatatu katika sehemu ya tatu na ya mwisho ya mada hii. Mimi na wewe ni ndugu, au siyo?
Mungu mpaji wa viumbe vyote, ndiye aliyetoa fursa hii kwangu, ili niitumie kama mwangaza kwako ndugu yangu. Namshukuru sana kwakuwa yeye ndiye kila kitu katika maisha yangu.

Tupo kwenye sehemu ya tatu na ya mada hii inayosema: “Simu, mitandao ya kijamii, vinawatesa wengi.” Twende kazi msomaji wangu, kuna kitu kikubwa cha kukusaidia utakachokipata baada ya hapa.
Hebu jiulize, wapenzi wanatengana, wanandoa wanakosa suluhu, kwa sababu ya sms au simu. Baadhi wanaishi katika uhusiano wa ‘ilimradi siku zinaenda’, yaani ni mashaka tupu.

Wengine hawana amani, wanawapiga marufuku wenzi wao kushika simu zao au kuzizima muda wote, yote kwa yote ni kukwepa nyeti zao za kucheza mechi za nje, zisigundulike.
Lipo pia, lile kundi ambalo ‘husevu’ majina ‘feki’ katika simu zao ili wasishtukiwe, Husna kuitwa Hussein, Nasra kuandikwa Nassor au Jane kama John. Mwanamke kumuandika Joseph kama Josephine, hivyo ni vijimambo tu!

Kama utakumbuka vizuri katika kipengele cha kwanza cha mada hii iliyopita, niliandika ‘KUJIAMINI’. Hapo nilikuwa namaanisha kuwa kama kweli wewe ni muamifu, haina haja ya kujishtukia.
Wapo wenzangu na mimi ambao wakipigiwa simu, badala ya kupokea mbele ya wapenzi wao, wanaweza kufunga safari na kwenda kuongelea maili moja. Huu nao ni ufisadi wa mapenzi!

Daima ukiangalia simu zao, hutakuta sms yoyote, iwe kwenye inbox, outbox, sent item ama katika draft. Ukitazama incoming na outgoing calls, majina hayana mashaka, lakini maongezi yake ni kizaa zaa. 

Itaendelea wiki ijayo.

www.globalpublishers.info.

No comments: