
“HII ni moja ya changamoto ambazo sitazisahau katika maisha yangu. Imekuwa ni kazi kubwa, yenye shinikizo mbalimbali, kuna wafanyabiashara wanaoshawishi kupata tenda, lakini nashukuru Mungu mwishoni tumepata kampuni yenye viwango bora.”
Ilikuwa kauli ya utangulizi ya Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dickson Maimu alipokutana na wahariri na waandishi waandamizi wa habari katika Ilikuwa kauli ya utangulizi ya Mkurugenzi Mkuu wa
mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam asubuhi ya Jumamosi ya Desemba 10, mwaka huu.
Maimu aliitisha mkutano huo kuzungumzia maendeleo ya mradi huo wa vitambulisho vya
Taifa, ambao licha ya sheria kupitishwa takriban miaka 15 iliyopita, hadi sasa hakuna kitambulisho kilichotoka.
Mradi huo kama alivyoeleza Maimu, umekuwa na changamoto nyingi, shinikizo kutoka kwa
watu mbalimbali; viongozi wa Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine, kwa sababu
mbalimbali.
Lakini bila ya shaka, kutokana na ukweli kuwa una fedha nyingi. Hadi kukamilika kwake, inategemewa utagharimu kiasi cha Sh bilioni 350 za Serikali ya Tanzania na baadhi ya wabia
wa maendeleo.
Hivyo, haishangazi hata kidogo kuona kwamba unaumiza kichwa kwa mtendaji huyo mkuu, unawapeleka puta viongozi wa Serikali na hata baadhi ya wananchi wa kawaida. Lakini
hatimaye, kazi sasa imeanza na inatarajiwa kuwa ifikapo Aprili 26, mwakani, baadhi ya Watanzania watakuwa na vitambulisho hivyo.
Hao si wengine, bali ni watumishi wa Serikali ambao kwa muda mfupi sasa wameshaanza kazi ya usajili na utambuzi, baadaye kufanyiwa uhakiki wa taarifa zao na kisha kupatiwa vitambulisho vya Taifa.
“Leo hii tuko hapa kuwajulisha mafanikio ambazo Serikali kupitia Mamlaka ya Vitambulisho
vya Taifa imefanikiwa kutekeleza, ambazo ni kuanza kwa zoezi la utambuzi na usajili wa watu kwa ajili ya kupewa vitambulisho vya Taifa baada ya kipindi kirefu cha kusubiri kuanza kwa utekelezaji wa zoezi la utoaji wa vitambulisho vya Taifa,” alieleza Mkurugenzi Mkuu wa NIDA.
Kwa mujibu wa Maimu, kila Mtanzania atakuwa na kitambulisho cha Taifa kufikia mwaka
2015 ambacho kitatolewa bure na Serikali. Alisema baada ya wafanyakazi wa Serikali, watafuatiwa wanafunzi, wafanyabiashara na hatimaye umma kwa ujumla utafikiwa na kazi hiyo
muhimu kwa Taifa.
Maimu alisema ni lengo la Serikali kuhakikisha kila Mtanzania anakuwa na kitambulisho cha Taifa ifikapo mwaka 2015 na hilo litasaidia kuboresha Daftari la Kudumu la Wapigakura, na
hivyo kuipunguzia mzigo mkubwa Serikali katika kuboresha daftari hilo kila wakati wa uchaguzi unapowadia.
“Kwa kuwa zoezi la utambuzi na usajili litafanyika kwenye maeneo yenu nawaomba mtoe
ushirikiano wa kutosha kwa wananchi wote na niwakumbushe kuwa huduma hii ni bure kwa mujibu wa maagizo ya Baraza la Mawaziri, na hivyo Serikali haitarajii mtendaji yeyote kuomba au kupokea chochote au kuweka tozo.
“Tumeanza zoezi la usajili kwa watumishi wa umma, katika Wizara zote na Taasisi za Serikali.
Hivyo, tunawaomba wananchi hususani watumishi wa umma kutokubali kulipa gharama zozote katika usajili wa fomu zao pindi wanapokwenda kwenye ofisi za serikali za mitaa na kata
kwani zoezi hili halina tozo au gharama zozote anazopaswa kulipia wananchi,” alieleza Mkurugenzi Mkuu wa NIDA.
“Naomba kutumia fursa hii kuwafahamisha wananchi kwamba fomu za usajili bado hazijaanza kutolewa kwa wananchi wa kawaida, na utaratibu wa utoaji wa fomu hizo tutautangaza wakati wake utakapofika.
“ Tu n a w a s i h i wananchi na wageni, wasikubali kudanganywa au kulipa fedha zozotekwani kitambulisho ni bure na huduma zote zinazoambatana na zoezi hili ni bure. NIDA haitasita
kuchukua hatua za kisheria kwa ye yote atakayebainika kukiuka uratatibu huu, ” anafafanua
Maimu.
Anasema usajili umeanza kwa watumishi wa umma katika Wizara, Idara zinazojitegemea na Wakala za Serikali ikiwa ni hatua ya kwanza ya majaribio na kisha kuelekea kwa wananchi
wote kwa mujibu wa ratiba ya utekelezaji, na kwamba wameanza na kundi hilo kwa sababu vitambulisho kwao si tatizo kwa maana ya mfumo walionao una urahisi katika kuwashughulikia, lakini zaidi, itasaidia katika kudhibiti watumishi hewa.
“Hawa kwao kitambulisho kwao kidogo si tatizo, kwani wana mifumo mizuri na hawa tunataka
kuwatumia kama majaribio kwa mradi huo.
Lakini zaidi, itasaidia katika kudhibiti tatizo la watumishi hewa serikalini,” alisema Maimu na kuongeza kuwa watafuata wanafunzi kwa sababu ya kusaidia katika suala la mikopo ya elimu ya juu na kwa wafanyabiashara ili kudhibiti mianya ya ukwepaji kodi na kusaidia kuongeza mapato.
“Kutokana na ratiba yetu ya utekelezaji, tutaanza kutoa vitambulisho kwa awamu ya kwanza
mwezi Aprili 26, 2012 wakati wa maadhimisho ya sherehe za Muungano kwa watumishi wa
Serikali ambao tayari usajili umeanza,” alieleza Maimu na kuongeza kuwa katika utekelezaji
wa mradi huo, Mamlaka itatoa vitambulisho katika makundi matatu; Watanzania, wageni
wakazi na wakimbizi.
“Tutatoa vitambulisho hata kwa mwizi, kwa sababu moja ya faida kuu za mradi huu ni kudhibiti
suala la usalama wetu kwa kila pointi. Ndiyo maana dhana kuu ya mfumo huu inatakiwa ijibu maswali makuu manne; nani ni nani; yuko wapi; anamiliki nini na anafanya nini?”anaeleza.
Aliongeza kuwa vitambulisho hivyo katika eneo la usalama, vitasaidia kuimarisha usalama wa
raia na mali zao na kupunguza vitendo vya uhalifu na hasa unaofanywa na raia kutoka nchi
jirani na wafungwa waliomaliza adhabu zao au kuachiwa huru kwa msamaha wa Rais.
“Ni wazi kuwa udhibiti wao umekuwa mgumu kutokana na kushindwa kuwatambua. Pia itasaidia kuweka kumbukumbu za matukio ya uhalifu katika daftari,” alisema Mkurugenzi Mkuu wa NIDA.
Alisema baada ya usajili kukamilika, jukumu kubwa litakalofuatia ni uhakiki wa taarifa za makazi, umri na uraia wa mwombaji aliyesajiliwa ili kupata uhakiki wa taarifa zake kwa lengo
la kumpatia kitambulisho kinachowiana na kundi lake.
Katika udahili, mwombaji atatakiwa kuthibitisha kama amekuwa akiishi Tanzania kwa kipindi kisichopungua miezi sita; uthibitisho wa umri wa miaka 18 na uthibitisho wa uraia wake. Aidha, viambatanisho muhimu vitahitajika ambavyo ni cheti cha kuzaliwa; cheti cha ubatizo/falaki; kitambulisho cha Mpigakura; pasipoti ya Tanzania na cheti cha kuhitimu elimu ya msingi.
Ili kufanikisha kazi hiyo, anasema wanashirikiana kwa karibu sana na Serikali za Mitaa kwa
lengo la kutambua makazi halali ya mwombaji; Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kwa lengo la kutambua umri wa mwombaji na Idara ya Uhamiaji kutambua na kubaini uraia wa
mwombaji.
“Kwa uelewa huu, tunaomba snaa watendaji wote wa Serikali za Mitaa wasaidie zoezi la utambuzi na usajili wa watu kwenye maeneo yao. Naomba nitoe rai kwa watendaji kuwa tuwe wazalendo na waadilifu wakati wa utekelezaji wa zoezi hili, tuepuke vitendo vyovyote vya rushwa pamoja na ukiritimba wowote unaopelekea kudai au kupokea rushwa,” anasema Maimu na kuongeza: “Jukumu hili ni la muhimu sana na linatakiwa kufanywa kwa umakini mkubwa bila kuharakishwa kwani uharaka kidogo tu unaweza kabisa kuharibu zoezi zima.”
Maimu anazitaja faida za mfumo wa Taifa wa utambuzi na usajili wa watu kwamba zinasaidia
kupata taarifa sahihi katika maeneo ya kiuchumi, kijamii na kiusalama.
“Utekelezaji wa mradi huu umekuja wakati muafaka ambao nchi yetu ni mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, na karibu nchi zote katika umoja huu tayari wana vitambulisho vya Taifa.
Hivyo, kwa Tanzania zoezi hili limekuja wakati muafaka katika ushindani wa soko huria na
mpango wa Soko la Pamoja la Afrika Mashariki,” anasema Mkurugenzi Mkuu wa NIDA.
Anazitaja baadhi ya faida za jumla za mradi huu kwa Taifa kuwa ni vitambulisho hivyo kusaidia
kuimarisha usalama wa raia na mali zao na kupunguza vitendo vya uhalifu na hasa unaofanywa
na raia kutoka nchi jirani na wafungwa waliomaliza vifungo vyao au kuachiwa huru kwa msamaha wa Rais.
Kutokana na kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kitambulisho kitatumika
kusafiria kati ya nchi wanachama wa jumuiya, tofauti na sasa ambapo lazima msafiri kuwa na hati ya kusafiria; vitambulisho vya Taifa vitasaidia kuwasajili na kuwatambua wananchi ambao watanufaika na upatikanaji wa ruzuku za pembejeo za kilimo na hivyo kufanikisha
azma ya Kilimo Kwanza.
Faida nyingine ni kusaidia kumtambua mhusika anapohitaji kupatiwa huduma katika Taasisi
mbalimbali kama vile benki, taasisi za mikopo na huduma za afya; kuiongezea Serikali wigo wa ukusanyaji mapato na hivyo kuboresha huduma za kijamii kama vile afya, elimu, barabara pamoja na ulinzi na usalama wa raia na mali zao.
“Kuweka kumbukumbu za matukio ya watu wote katika daftari la utambuzi na usajili na hivyo
kuisaidia Serikali na Taasisi binafsi katika shughuli za kila siku na katika kupanga vipaumbele,”
anasema Maimu.
Anaitaja faida nyingine kuwa ni kusaidia kupunguza wafanyakazi hewa kwenye mfumo wa taarifa za kiutumishi na mishahara serikalini na kuhakikisha kuwa wananchi wanapata stahili
zao za kijamii; kwa mfano kupata malipo ya pensheni, haki za matibabu, haki za kujiunga na masomo ikiwa ni pamoja na stahili zote ambazo raia wa Tanzania anastahili.
Mkurugenzi Mkuu huyo anasema kuwa katika Mkutano ujao wa Bunge, wanatarajiwa utapelekwa muswada wa mabadiliko ya sheria ambayo itakuwa ni lazima kwa kila mtu anayeishi nchini, kuwa na kitambulisho hicho cha kudumu ambacho kadi yake itakuwa ni ya
miaka 10.
NIDA imeingia mkataba na mkandarasi wa vitambulisho hivyo, Kampuni ya IRIS Corporation
Berhad ya Malaysia tangu Aprili 21, mwaka huu.
Mshauri mwelekezi wa mradi huo ni Kampuni ya Gotham International Ltd (GIL), na tayari Mamlaka hiyo imepata viwanja katika wilaya zote nchini kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya ofisi za usajili wilayani wakati kituo kikuu cha kuhifadhi takwimu zote za nchi kitakuwa Kibaha, Pwani.
Maimu alisema kulikuwa na uchelewaji wa kutoa fedha kwa mkandarasi kuanza kazi, lakini
tayari Oktoba mwaka huu amekabidhiwa fedha hizo baada ya kuidhinishwa na Bunge na tayari
ameleta mashine kuanza kazi ya mradi huo uliosubiriwa kwa zaidi ya miaka 15 sasa na ukagubikwa na mambo mengi katika mchakato wake.
Lakini kwa hatua hiyo, sasa ni dhahiri kwamba vitambulisho vya Taifa vilivyosubiriwa kwa muda mrefu na kuonekana kama ni ndoto, ni jambo linalowezekana na wakati Watanzania
watakapokuwa wanaadhimisha miaka 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, baadhi
watakuwa na vitambulisho hivyo mifukoni mwao.
Habari Leo
No comments:
Post a Comment