![]() |
| Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed |
Chama cha Wananchi (CUF) kimepeleka taarifa Bunge kuliarifu kuhusu uamuzi wa kufukuzwa uanachama kwa Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed, uliochukuliwa na Baraza Kuu la Uongozi wa Chama hicho Taifa, Januari 4, mwaka huu.
Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Ismail Jussa Ladhu, alisema jana kuwa taarifa hiyo ilipelekwa Bunge jana ili kulitaka liiarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwamba, itangaze kwamba jimbo hilo liko wazi kutokana na Hamad kufukuzwa uanachama.
Hata hivyo harakati za Hamad zimezidi kukichanganya Chama cha Wananchi (CUF), ambacho jana kwa mara nyingine kiliibuka na kuziita taarifa za wanachama zaidi ya 1,000 wa mikoa ya Dar es Salaam na maeneo mengine kurudisha kadi za chama hicho zilizotolewa na mbunge huyo juzi kuwa ni za uongo na propaganda.
Kauli hiyo ya CUF ilitolewa na Mkurugenzi wake wa Haki za Binadamu na Uenezi, Amina Mwidau, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotumwa kupitia mtandao wa kompyuta jana.
Mwidau, ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum (CUF) alisema katika taarifa hiyo kuwa CUF imefuatilia na kubaini habari hizo kuwa ni za uongo na propaganda zinazoenezwa na Hamad.
Alisema kadi zinazoonyeshwa na Hamad kwa waandishi wa habari si za wanachama, bali ni za kutengenezwa.
Mwidau alisema kadi ziliandaliwa na Hamad wakati wa kura za maoni za kuwapata wagombea wa ubunge na uwakilishi kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 na chama kikazuia uingizaji wa wanachama wapya muda mfupi kabla ya kura hizo.
“Kwa wakati huo Hamad alikuwa ameandaa kadi mpya 7,000 ziweze kumsaidia katika kinyang’anyiro hicho,” alisema Mwidau.
Aliongeza: “Hivyo basi hakuna wanachama 1000 waliompelekea kadi kwani wanaCUF wako ngangari na chama kipo imara kwa kuwa wanatambua kuwa wao si wanachama wa UHS (United Hamad Suppoters), bali wao wanachama wa The Civic United Front hivyo hawapo kwa maslahi ya mtu binafsi.”
Alisema kumekuwa na zoezi la kununua kadi za wanchama wa CUF alikodai kuwa kunafanywa na Hamad kwa kutumia watu mbalimbali.
Hivyo, akawataka wanachama kutokubali kutoa kadi zao kwa namna yoyote na kwa mtu yeyote.
Juzi akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam, Hamad alisema anaamini wanachama wa CUF popote walipo wameguswa na uamuzi wa kuvuliwa uanachama uliochukuliwa na Baraza Kuu dhidi yake na wenzake wanne.
Alisema Jumatano wiki hii wanachama wa CUF mkoani Tanga walimweleza wamekwisha kufikisha kadi 100 kukusanya, huku Wilaya ya Temeke wakiwa wamekusanya kadi 600 na Mwanza wakiandaa maandamano makubwa.
“Tanga wameniambia mpaka jioni leo (juzi) watakuwa na kadi 2,000, Mwanza sijui zitakuwa ngapi, Morogoro wamenipigia simu hawajui ngapi,” alisema Hamad.
Katika hatua nyingine, alisema CUF itakuwa na mkutano wa hadhara katika viwanja vya Barafu-Manzese, kuanzia saa 7 mchana leo.
Mwidau alisema mkutano huo utahutubiwa na Katibu Mkuu wa CUF, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.
Alisema mkutano huo utahudhuriwa pia na viongozi wote wa CUF Taifa isipokuwa Mwenyekiti, Profofesa Ibrahim Lipumba, ambaye yuko Marekani kwa kazi za kimataifa.
Mwidau alisema mkutano huo utatoa ufafanuzi wa kina juu ya maamuzi ya Baraza Kuu la Uongozi wa CUF Taifa yaliyofikiwa katika kikao chake kilichofanyika hivi karibuni mjini Zanzibar na pia uta pamoja utaelezea mustakabali wa chama na hali ya umaskini unaoikabili nchi.

CHANZO: NIPASHE
.jpg)
No comments:
Post a Comment