Ndugu watanzania waishio PA, DE, MD, DC, na popote Marekani.
Kwa niaba ya familia ya Mrema wa Moshi na Mwanza tunatoa shukrani zetu kwa michango yenu ya hali na mali ambayo ilituwezesha kuandaa na kusafirisha mwili wa marehemu Steina Mrema kwenda nyumbani Moshi kwa mazishi.
Mwili wa marehemu uliwasili salama Kilimanjaro Tanzania, Jumatano tarehe 4 Januari 2012 pamoja na mtoto wa marehemu na mama mtoto. Mazishi yalifanyika Alhamisi tarehe 5 Januari 2012. Marehemu alizikwa nyumbani kwa wazazi wake Moshi vijijini.
Tunatoa shukrani maalum kwa kanisa la Cathedral of Praise la Lanham Maryland kwa kuandaa misa ya kumuaga ndugu na kaka yetu Steina. Vilevile shukrani maalum kwa nyumba ya mazishi ya Donaldson kwa kuandaa na kuhifadhi mwili wa marehemu wakati tukifanya maandalizi ya kuusafirisha kwenda nyumbani.
Imekuwa vigumu kumshukuru kila mtu aliyejitoa mchango lakini ujumbe huu utakuwa umewafikia wote kwa njia ya mtandao.
Ni vigumu kukubali kwamba ndugu yetu na mwanajumuia yetu ametutoka kwa ghafla. Ndugu yetu ametuachia pengo ambalo kamwe hatutaweza kuliziba.
Tunamwomba Mungu awazidishie mara dufu ya kile mlichotoa.
Asanteni na Mungu awabariki.
Wanakamati ya maandalizi ya Mazishi.
1 comment:
RIP BRO, I LOVE YOU FOREVER.
Post a Comment