
Mshambuliaji wa Timu ya Sudan,Mudather Elteib.Sudan inacheza mechi ya robo fainali leo dhidi ya Zambia
AFRIKA inasumbili kushuhudia miujiza mingine kwenye robo fainali ya Mataifa ya Afrika, wakati Sudan itakapoikabili Zambia na wenyeji Equatorial Guinea dhidi ya Ivory Coast.Sudan na Equatorial Guinea ni timu mbili zilizoshangaza ulimwengu kwa kufanikiwa kufika hatua hiyo kubwa ya mashindano hayo.
Wawakilishi wa Afrika Mashariki, Sudan wamefuzu kwa kuwafunga Burkina Faso (2-1) ukiwa ni ushindi wao wa kwanza tangu walipochukua ubingwa mwaka 1970, walitoka sare 2-2 na Angola huku wakifungwa 1-0 na Ivory Coast kwenye mchezo wa ufunguzi ya Kundi B.
Sudan wanajivunia ubora wa ligi ya kwao na wachezaji wote kujuana kutokana na kucheza soka nchini humo, lakini wanategemea kupata upinzani mkali kutoka kwa Zambia inayosifika kwa soka lao la kushambulia kwa nguvu.
Zambia wamethibitisha ubora wao kwa kumaliza vinara wa Kundi A na Chipolopolo wanasaka kufuzu kwa nusu fainali kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1996.
Zambia wamethibitisha ubora wao kwa kumaliza vinara wa Kundi A na Chipolopolo wanasaka kufuzu kwa nusu fainali kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1996.
Kocha wa Zambia, Herve Renard amesema Sudan hawezi kuwazuia kutimiza lengo lao la kucheza nusu fainali.
Renard amekiri kuwa mechi hiyo itakuwa nguvu kwa Zambia, lakini Chipolopolo hawana la zaidi ya kuifunga Sudan.
Renard amekiri kuwa mechi hiyo itakuwa nguvu kwa Zambia, lakini Chipolopolo hawana la zaidi ya kuifunga Sudan.
Wenyeji Equatorial Guinea nchi ilisiyokuwa na jina kwenye ulimwengu wa soka, watashuka dimbani kwa lengo la kuendelea kuuduwaza ulimwengu kwa kuwatoa Didier Drogba na Yaya Toure kwenye robo fainali ya Kombe a Mataifa ya Afrika.
Wenyeji hao wenza wamekusanya wachezaji waliozaliwa na kukulia Hispania kwa wazazi wao ni wenyeji wa nchi hiyo, wengine wamewapa uraia tayari wameshawangaza wengi kwa kufika robo fainali.
Watakuwa wakijaribu kufanya muujiza mwingine kwa kuondoa mashindano Ivory Coast iliyoshinda mechi zake zote tatu bila ya kufungwa bao lolote.
“Hatujioni kama timu ndogo,” kocha wa Equatorial Guinea, Gilson Paulo aliimbia Reuters. “Japokuwa vyombo vya habari wanatuona kama timu dhaifu, lakini lengo letu ni kwenda mbali zaidi iwezekanavyo.”
Katika mechi nyingine wenyeji Gabon, wanategemea kasi ya mshambuliaji wao Pierre-Emerick Aubameyang watakapomvaa Seydou Keita na Mali na huku wakishangiliwa na mashabiki wao wa nyumbani itawasaidia kufuzu.
Ghana wanaopewa nafasi ya kucheza fainali watajaribu bahati yao kwa Tunisia timu isiyotabilika.
Ghana wanaopewa nafasi ya kucheza fainali watajaribu bahati yao kwa Tunisia timu isiyotabilika.
Mashindano hayo yalionekana kama si kitu baada ya Nigeria, Cameroon, Afrika Kusini na Misri kushindwa kufuzu, lakini hali imekuwa ni tofauti na kuwa moja ya fainali bora zaidi hivi karibuni kwa matokeo ya kuvutia.
Kumekuwa na mabao mengi ya kuvutia, pamoja na yale ya mashuti ya mbali na magoli ya dakika za mwisho kama lile la Gabon walilofunga dakika 95 na kuitoa Morocco 3-2 na kufuzu kwa robo fainali.
Jambo jingine ni viwanja kuwa vyeupe wakati wenyeji wanapokuwa mapumzikoni japokuwa uwanja wa Nuevo de Malabo unaochukua mashabiki 15,000, leo utaonekana mdogo wakati Equatorial Guinea watakapowakaribisha mabingwa wa mwaka 1992 Ivory Coast.
Kuifunga Ivory Coast inaoneka kuwa ni mtihani mkubwa kwa wenyeji hao ambao walifuzu kwa kuzifunga Libya na Senegal.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment