IJUMAA ya Januari 27, mwaka huu, ni siku ambayo Hamisi Kijanga
anasema hawezi kuisahau katika maisha yake.
Ilikuwa ni siku iliyobeba kitu kipya katika utumishi wake akiwa kama dereva kwa kipindi cha miaka 35, ilikuwa ni katika sherehe ya kumuaga Mkuu wa Mkoa (mstaafu) Dk James Msekela, kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Rehema Nchimbi na kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tuppa.
anasema hawezi kuisahau katika maisha yake.
Ilikuwa ni siku iliyobeba kitu kipya katika utumishi wake akiwa kama dereva kwa kipindi cha miaka 35, ilikuwa ni katika sherehe ya kumuaga Mkuu wa Mkoa (mstaafu) Dk James Msekela, kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Rehema Nchimbi na kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tuppa.
“Tukio ambalo sitalisahau maishani mwangu ni kitendo cha Tughe Taifa
kunizawadia cheti cha utumishi bora. Nilijisikia furaha kubwa kwa
sababu tangu nianze kuendesha viongozi sijawahi kupata ajali na hata
ninapoachia gari naiacha katika hali nzuri, ni faraja na heshima kubwa
kwangu pamoja ya familia yangu,” anasema.
Kulingana na maelezo yake, alianza rasmi kazi ya udereva mwaka 1977 kwenye ofisi ya Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mkoa wa Dodoma wakati huo akiwa upande wa ujenzi na alikuwa akiendesha magari makubwa ya kubeba changarawe wakati wa ujenzi wa barabara.
Aliingia kazini baada ya kutoka Chuo cha Ufundi Chang’ombe, Dar es Salaam, mwaka 1976 lakini ilipofika mwaka 1985 alihamishiwa kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, ambapo alianza kazi kwa kumuendesha Katibu tawala Msaidizi, Japhet Kamala ambapo alimuendesha kwa muda wa miezi sita na kuteuliwa kumuendesha Mkurugenzi wa Maendeleo wa Mkoa, Danford Mapunda.
Alimuendesha Mkurugenzi huyo hadi mwaka 1987 mwanzoni na katikati ya mwaka 1987 aliteuliwa kumuendesha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma wakati huo Athumani Kabongo hadi mwaka 1993. Kuanzia mwaka 1993 hadi 1995 alikuwa akimuendesha Mkuu wa Mkoa, William Kusila.
Mwaka 1995 hadi 2003 alimuendesha Isdory Shirima, mwaka 2003 hadi 2006 alimuendesha Alhaji Mussa Nkhangaa, 2006-2009 alimuendesha William Lukuvi, 2009 hadi 2011 alimuendesha Dk. James Msekela na 2011 hadi sasa anamuendesha Dk. Rehema Nchimbi.
Mbali na kutumiza wajibu wake vizuri akiwa kama dereva anasema kuwa, tukio ambalo hataweza kulisahau Kijanga anabainisha kuwa kati ya mwaka 2001 au 2002 wakati akimuendesha Mkuu wa Mkoa wakati huo alikuwa Isdory Shirima walivamiwa na majambazi wenye silaha lakini kwa ujasiri wake aliweza kumuokoa Mkuu wa Mkoa.
Wakati huo walikuwa wakitoka ziara Dodoma Vijijini na walipofika njiapanda ya Bihawana na Iringa, walitekwa na majambazi licha ya kuwa walikuwa kwenye msafara wa magari saba.
“Pia tulikuta magari mengine kama sita ambayo pia yalikuwa yametekwa
na abiria walitolewa na kwenda kufungiwa kwenye lori,” anasema.
Anasema kuwa, yeye binafsi aliporwa shilingi 60,000 pamoja na saa ya
mkononi aina ya Citizen yenye thamani ya shilingi 80,0000 na pia watu
wengine waliporwa fedha na simu za mkononi, saa na vitendea kazi vya
kiofisi.
Akisimulia jinsi walivyookoka katika ajali hiyo, alisema kuwa alitumia ujasiri ili kuokoa viongozi waliokuwa nao wajifiche kwa kuwashawishi
kuingia porini.
“Walitutoa na kutufungia kwenye lori bahati nzuri tulikuta watu wamejaa wakafunga mlango katika kuhangaika kujiokoa kumbe mlango haukubana tukaufungua na kutoka tukakuta majambazi yakiw a yameondoka,” anasema.
Anasema kuwa, alipofika karibu na gari akaangalia sehemu aliyotupa ufunguo akokota na kufungua gari wakati huo mabosi wake bado walikuwa maporni, akafungua gari na kuwaambia kuwa watoke maporini
kwani majambazi yalikuwa yameondoka ndipo walipokwenda kuripoti katika kituo cha polisi.
Akielezea tatizo la ajali anasema kuwa, ajali nyingi zinasababishwa na
kutofuata kanuni za udereva. Akieleza historia ya maisha yake, anasema kuwa, alizaliwa Kaliua Mkoani Tabora, mwaka 1960, kwenye familia ya watoto sita ya mzee Nassoro Kijanga na mama Mwajeni Saidi, ambao wote bado wako hai.
Alisoma shule ya Msingi Kaliua hadi darasa la sita na kuhamia mkoani
Dodoma, kumfuata baba yake ambaye wakati huo alikuwa dereva katika
Wizara ya Ujenzi.
Alisoma katika shule ya msingi Mlimani katika Manispaa ya Dodoma na mwaka 1975 alimaliza darasa la saba, lakini hata hivyo hakuweza kuchaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari na kwenda Chuo cha Ufundi Chang’ombe, Dar es Salaam kwa ajili ya kusomea ufundi.
Mchenya John ni Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na
Afya Tanzania (TUGHE), anasema kuwa kama chama wanatambua juhudi za wafanyakazi moja kwa moja wanaojituma zaidi katika utendaji kazi wafanyakazi, kazi yao ni kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi wa ngazi zote.
Anasema kuwa Mchenya amepewa tuzo, si tu kwa ajili ya kuendesha Wakuu wa mikoa saba, bali kwa ajili ya kuipenda kazi yake na majukumu yake pia ni mtu anayezingatia maadili ya kazi yake, pia ni mtunzaji mzuri wa magari ya Serikali kwani magari aliyokuwa akikabidhiwa tangu alipoaanza kuendesha wakuu wa Mikoa mwaka 1987 hakuwahi kupata ajali wala kuharibu gari alilokabidhiwa na matokeo yake amekuwa na sifa za kukabidhi gari alilokuwa nalo likiwa katika hali nzuri.
Mchenya anasema kuwa TUGHE waliona ni busara wakati wanafanya tendo la kutambua na kuthamini uteuzi wa viongozi katika Mkoa wa Dodoma ni vizuri kushirikisha wanachama wa kada zote katika kuthamini na kutambua juhudi zao.
“Tuliona ni wakati muafaka wa kumtunukia dereva huyo kama mfano bora
wa kuigwa kwa watumishi wengine wa ngazi ya kawaida ili kuthibitisha
hatambui watu wa ngazi za juu tu ndipo chama kimemtunuku hati ya
kutambua na kuthamini mchango wake, pia alipewa zawadi ya kitambaa cha suti na kitenge cha wax kwa ajili ya mkewe,” alisema.
Aidha Mchenga alitoa changamoto kwa waajiri kuthamini juhudi
zinazofanywa na wafanyakazi wa ngazi zote.
HABARI LEO
No comments:
Post a Comment