Pastor Alan DeSilver akiendesha ibada ya kumuaga mpendwa wetu, Christavina Cryor kwenye kanisa la Seventh Day Adventist, lililopo Takoma Park, Maryland, Mtaa wa Carroll.
Mume wa Marehemu, Lavorn Cryor akiongea machache kuhusu Christavina huku akiwa amembeba mtoto wao mdogo ambae alifikisha miaka 2 siku mbili baada ya kifo cha mama yake.
Kaka ya Marehemu, Boaz Kusaga akiongea machache kuhusu Christavina.
Michelle Hyason, mfanyakazi mwenzake na marehemu akiongea machache kuhusu Christavina.
Teddy Gallus, Rafiki ya marehemu akiongea machache kuhusu Christavina.
Shukurani Magoma, shemeji ya marehemu akisoma wasifu wa Christavina.
Kutoka kushoto ni Ghati Matinyi, Vickie Keita na Deborah Chemkaka wakiimba wimbo maalum kwa ajili ya marehemu.
Kushoto ni Mama mzazi wa Christavina aliyekuja toka Tanzania akiwa pamoja na Mume wa marehemu, Lavorn Cryor.
Kaka ya marehemu, Boaz Kusaga akiwa na Mama mzazi.
Kushoto ni Dada ya marehemu akiwa amembeba mwanae, mtoto wa kwanza wa Christavina wakiwa pamoja na mdogo wa marehemu.
Ndugu, marafiki na jamaa waliofika kwenye Ibada hiyo.
Ndugu na marafiki wa karibu na familia wakisaidia kuwaongoza Watanzania, ndugu, jamaa na marafiki waliofika kwenye Ibada ya kumuaga Christavina Cryor.
Mmoja ya Watanzania kitia saini kitabu cha wageni.
Jamaa na marafiki wakitoa mkono wa pole baada ya kutoa heshima za mwisho.
kwa paicha zaidi Bofya Read More
2 comments:
Hii yote sababu ya ushirikiano,bila hivyo hata haya sasa tusingeyaona Dj luke endeleza upendo huo na wote waliojitolea kwa majukumu mbalimbali mungu awabariki siku zote tunasema umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu,tafakarini jamani,na kutoa ni moyo.
kwa kweli inatia huruma sana ila kwa kuwa MUNGU ameruhusu nasi hatuna budi kukubali ya kuwa mapenzi yake yatimizwe kwetu nasi tulio baki hai Mdogo wangu BOAZI Mungu akutie nguvu sana na uwe na moyo mkuu siku zote za maisha yako
Post a Comment