Sehemu ya kwanza ya makala haya wiki iliyopita nilieleza kuwa upendo ni kipengele kikuu. Unaweza kukiita kifungu mama ndani ya katiba ya mapenzi. Huwezi kusema upo kwenye uhusiano makini kama upendo haupo katikati.
Chukua hatua madhubuti endapo utabaini upendo haupo. Mkatae mwenzi ambaye hakupendi, kinyume chake atakupa mateso mbele ya safari. Kuna faida kubwa mbele ya safari endapo utamkataa asiyekupenda au usiyempenda leo, kuliko kumng’ang’ania, kwani itakutesa.
Muongozo wa kipengele cha upendo ni kwamba lazima wewe mwenyewe uanze kuwekeza kisha naye akupende. Ni maisha ya ubinafsi kutaraji kupendwa wakati wewe huoneshi kwa mwenzako. Zingatia hili kila siku na wakati wote ili uweze kufaidi matunda mema kwenye uhusiano wako.
Kuna tabaka la watu ambao huishi kwa kusikilizia zaidi. Haitakiwi kutegea, upendo unamaanisha pande mbili zinazovutana. Huyu anatekeleza hili kwa ajili ya mwenzake, hali kadhalika na mwingine anasimama imara kuhakikisha mpenzi wake anafaidi malisho mema ya huba. Hakikisha mpenzi wako hakushindi upendo, onesha unampenda zaidi.
Upendo huyeyusha mengi. Ukiwekeza upendo kwa mwenzi wako, utamfanya nafsi yake iwe na woga. Ni rahisi kushinda vishawishi, kama atakuwa akikaa peke yake atakuwa akijiridhisha kuwa unampenda kwa moyo wako wote. Vinginevyo, anaweza kushawishika na kukusaliti kama tu akili yake itamtuma kuamini humpendi.
Hivyo basi, hakikisha upendo wako si wa wasiwasi. Mfanye awe na imani, ikibidi iwe ya kupitiliza. Utafiti unaonesha kuwa mtu aliyeonesha upendo mkubwa kisha akasaliti kwa tamaa zake, anapobainika na kuachwa hujuta zaidi kuliko yule aliyeona hakukuwa na upendo kwa sababu haoni cha kupoteza.
1.HOFU
Wengi hawajui hili. Unaweza kuwa na upendo mkubwa kwa mwenzi wako lakini kama huna hofu juu yake ni sawa na bure. Katika kipengele hiki, nashauri watu kujitenga na maneno yasiyo na faida. Mapenzi siyo tamko la kinywa peke yake, moyoni ndimo mahali pake.
Wengi hawajui hili. Unaweza kuwa na upendo mkubwa kwa mwenzi wako lakini kama huna hofu juu yake ni sawa na bure. Katika kipengele hiki, nashauri watu kujitenga na maneno yasiyo na faida. Mapenzi siyo tamko la kinywa peke yake, moyoni ndimo mahali pake.
Hii inamaanisha kuwa mapenzi hayatamkwi midomoni na yakaisha. Ni lazima mwili mzima uhusike kivitendo. Mantiki hapo ni kuwa unaweza kusema unapenda lakini kama huna hofu yoyote kwa huyo umpendaye ni sawa na kupiga gitaa kumtumbuiza mbuzi, kwani hakutakuwa na matokeo mazuri.
Faida ya hofu kwenye uhusiano ni kuwa kila nukta, dakika, saa na siku, utaishi kwa tahadhari. Lile ambalo unajua haliwezi kumpendeza mwenzi wako, hutalitenda, hivyo kufanya maelewano kuwa makubwa zaidi. Husaidia kuepusha migogoro na kuumizana bila sababu za msingi.
Kiburi kimejikita kwenye vichwa vya watu wengi, hivyo kufanya hata yale ambayo wapenzi wao hawataki. Mathalan, mtu anaweza kutambua kuwa akivaa nguo za aina fulani, mpenzi wake hawezi kufurahi lakini kwa sababu ya kutokuwa na hofu, anavaa na kuibua ugomvi usio wa lazima.
Mtu anajua kwamba mwenzi wake hapendelei tabia ya kutembea usiku lakini kwa sababu ya kiburi, anasaga rumba mpaka usiku wa manane ndiyo anarudi nyumbani. Ni kutafuta shari, hiyo ni tabia ya kutopenda amani na mwenzi wako. Sisemi uogope ila unatakiwa uwe na hofu kutoka moyoni.
Kila jambo linalotokea, hebu jiulize mara mbili mpaka tatu. Ukiona ni zito, jipe muda zaidi wa kutafakari kabla hujaamua. Inawezekana ukalichukulia ni dogo, kumbe mwenzako akalitafsiri kwa undani zaidi, mwisho akaona muachane kwa sababu amehisi unamdharau. Zingatia kwamba kufanya jambo la kumkera mpenzi wako kwa makusudi ni dharau.
Kila jambo linalotokea, hebu jiulize mara mbili mpaka tatu. Ukiona ni zito, jipe muda zaidi wa kutafakari kabla hujaamua. Inawezekana ukalichukulia ni dogo, kumbe mwenzako akalitafsiri kwa undani zaidi, mwisho akaona muachane kwa sababu amehisi unamdharau. Zingatia kwamba kufanya jambo la kumkera mpenzi wako kwa makusudi ni dharau.
Mimi kama mchambuzi wa masuala ya mapenzi, nimegundua baada ya utafiti wangu kuwa asilimia kubwa ya migogoro kwenye mapenzi hutokea kwa sababu ya wawili wanaoamua kupendana kukosa hofu. Hoja hapa ni kwamba ukiishi kwa kujiamini kupita kiasi mbele ya mwenzi wako ni janga. Ni sawa na kuuweka uhusiano wenu hewani.
Sina maana kuwa watu wasijiamini, mantiki ni kwamba kila mmoja ajipe hofu kwenye matendo yake ili asimkere mwenzake. Ajue kuwa dogo linaweza kuhatarisha mapenzi, kwa hiyo hatakiwi kuthubutu kutenda. Uhusiano wa kimapenzi huunganisha pande mbili zenye matarajio ya furaha, kwa hiyo ni vizuri kuishi kwa kuheshimu matarajio hayo.
Itaendelea wiki ijayo.
Itaendelea wiki ijayo.
www.globalpublishers.info
No comments:
Post a Comment