
Zamalek Yanga
Mwandishi Wetu
MABINGWA wa Tanzania, Yanga huenda wakacheza mechi yao ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zamalek nchi Sudan baada ya Misri.
MABINGWA wa Tanzania, Yanga huenda wakacheza mechi yao ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zamalek nchi Sudan baada ya Misri.
Uwezekano huo wa Yanga kucheza Sudan umekuja baada ya Shirikisho la Soka la Sudan(SFA) kupeleka maombi rasmi kwa Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) kutaka kuruhusiwa kuwa mwenyeji wa mechi zote zinazohusu klabu nne za Misri kwenye mashindano hayo ya Afrika.
Klabu nne za Misri zinazoshiriki Ligi ya Mabingwa na pamoja na Kombe la Shirikisho Afrika ni Al Ahly, Zamalek, Ismaily na ENNPI .
Masuala yote yanayohusu soka nchini Misri yamesimamisha kutokana na tukio za vurugu za mashabiki zilizotokea Port Said wiki iliyopita na kusababisha vifo vya watu 70 na mamia kujeruhiwa.
SFA tayari imeshaanza maandalizi ya kuwa mwenyeji wa mechi hizo zitakazofanyika wiki ijayo, lakini bado wanasubiri uamuzi wa mwisho wa CAF wa suala hilo.
SFA tayari imeshaanza maandalizi ya kuwa mwenyeji wa mechi hizo zitakazofanyika wiki ijayo, lakini bado wanasubiri uamuzi wa mwisho wa CAF wa suala hilo.
Taarifa hiyo ni habari njema kwa Yanga ambao tangu kutokea kwa vurugu hizo imekuwa ikihaha kuitaka CAF kubadili uwanja wataokocheza mechi yao ya marudiano Zamalek kwa ajili ya usalama.
Hata hivyo, Sudan inaweza kuwa si sehemu salama sana kwani mwaka 2009 wakati wa mechi ya mwisho ya kufuzu kwa Kombe la Dunia 2010 iliyozikutanisha Misri na Algeria kulitokea vurugu na mamia ya mashabiki kujeruhi.
Wakati huohuo, mwamuzi Israel Mujuni wa Tanzania ameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuchezesha mechi ya marudiano ya raundi ya mchujo ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya APR ya Rwanda na Tusker ya Kenya itakayochezwa jijini Kigali kati ya Machi 2, 3 na 4 mwaka huu.
Ofisa habari wa TFF, Bonifance Wambura alisema Mujuni atasaidiwa na Samuel Mpenzu na Khamis Maswa kutoka Tanzania wakati mwamuzi wa akiba katika mechi hiyo namba 18, atakuwa Louis Hakizimana wa Rwanda huku Kamishna wa mchezo huo atakuwa Aboubacar Nkejimana kutoka Burundi.
"Timu ya Mafunzo ya Zanzibar katika mechi yake ya kwanza katika raundi ya mchujo ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Muculmana de Maputo ya Msumbiji itakayofanyika mjini Zanzibar kati ya Februari 17, 18 na 19 mwaka huu itachezeshwa na waamuzi kutoka Shelisheli." alisema Wambura
Alisema Bernard Camille ndiye atakayekuwa mwamuzi wa kati akisaidiwa na Steve Marie na Gilbert Lista. Mwamuzi wa akiba katika mechi hiyo namba 27 atakuwa Ramadhan Ibada wa Tanzania wakati Kamishna atakuwa Ali Waiswa kutoka Uganda.
Kwa mujibu wa CAF, timu 13 bora zenyewe zimeingia moja katika raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
No comments:
Post a Comment