Mwana Libeneke wa jestina-george.com (kulia) akiwa katika pozi na mwanadada Safina Kassu wa Kassu Entertainment ambaye ndiye aliyeandaa tour hiyo ya Tundaman.
Msanii Tundaman yuko nchini Uingereza kwa ajili ya shoo iitwayo 'Tundaman Valentine Tour' iliyoandaliwa na mwanadada Safina Kassu wa Kassu Entertainment.
Shoo yake ya kwanza ilianza juzi tarehe Feb 11, 2012 katika kiota kipya cha maraha jijini London kiitwacho The Pit Stop 'Uwanja Wa Nyumbani' ambao msanii huyo alikonga nyoyo za mashabiki wake pale alipoanza makamuzi na kuwashukia na nyimbo zake pamoja na za kundi lake la Tip Top Connection.
Shoo zinaendelea na tunaomba watu wajitokeze kwa wingi kwa ajili ya kumsupport msanii na Mtanzania mwenzetu huyu.
No comments:
Post a Comment