ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, March 10, 2012

Siyoi Sumari, Nassari wapingwa Arumeru

Siyoi Sumari (CCM)                            Joshua Nassari (CHADEMA)
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimewasilisha pingamizi la uhalali wa uraia dhidi ya mgombea ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Siyoi Sumari, kikiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kumzuia mgombea huyo kushiriki ubunge katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki. 

Wakati Chadema wakimpinga Siyoi, Chama cha UPDP nacho kimewasilisha pingamizi dhidi ya mgombea wa Chadema, Joshua Nassari, ambaye jana alianza kampeni, kwa madai kwamba amejaza taarifa zake kwa ufupi na hajaweka wazi kazi anayoifanya kwa sasa. 


Aidha chama cha AFP nacho kimeungana na Chadema kupinga uraia wa Siyoi pamoja na udhamini wa wanachama waliojitokeza kumdhamini mgombea huyo wa CCM. 

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana, Msimamizi wa Uchaguzi wilayani Arumeru, Trasias Kagenzi alisema amepokea pingamizi tatu mbili kutoka chama cha AFP ambacho kimewasilisha pingamizi dhidi ya CCM kuhusu uhalali wa uraia wa Siyoi pamoja na udhamini wake kuwa na utata. 

Kagenzi alisema amepokea pingamizi hizo na wahusika watazifanyia kazi kisha majibu yatatolewa 

Alisema si kila pingamizi ni sahihi hivyo anapitia sheria kuona inasemaje na baada ya siku tatu au kabla ya siku tatu atatoa majibu ya wagombea waliowekewa pingamizi hilo. 

Juzi Kagenzi alibandika kwenye ubao wa matangazo uliopo kwenye jingo la Manispaa ya Arumeru na kwenye taarifa za Siyoi zilizobandikwa kwenye ubao wa matangazo zilisomeka kuwa alizaliwa Thika Mei 11, 1976 huko Nairobi, Kenya. 

Wagombea ambao hawajawekewa pingamizi ni Shabani Kirita (SAU), Mohammed Mohammed (DP) , Abrahamu Chipaka (TLP), Charles Msuya ( UPDP), Hamisi Kihemi (NRA) na Abdallah Mazengo

Habari Leo

No comments: