MWANAMKE mmoja ambaye ni raia wa Kenya, Njerika Kamau Msioka (20), amehukumiwa kutumikia kifungo cha miezi sita gerezani baada ya kukiri kosa la kuishi nchini kinyume cha sheria.
Mtuhumiwa huyo kwa maelezo yake alisema kuwa aliingia nchini mwaka 1992 na kuishi Jijini Dar es Salaam maeneo ya Tabata Bima.
Kwa mujibu wa Ofisa Uhamiaji wa Mkoa wa Dodoma, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Norah Massawe alisema kuwa, Februari 2, mwaka huu na alifukuzwa nchini kwa kusindikizwa hadi Namanga baada ya kubainika kuwa hana hati yoyote ya kumwezesha kuishi nchini.
Hata hivyo, alitoroka wakati anasubiri kurudishwa kwao katika kituo cha Namanga nchini Kenya na kurudi tena Tanzania hadi Dodoma.
Aidha Machi 8, mwaka huu, mwanamke huyo alikamatwa tena na ofisa uhamiaji mkoani hapa akiwa kwenye stendi ya mabasi ya Mohammed Trans iliyopo maeneo ya Uhindini akiwa na tiketi tayari kwenda mkoani Morogoro ambapo alifikishwa ofisi ya uhamiaji na kufunguliwa mashtaka ya kuingia na kuishi nchini kinyume cha sheria.
Alisema kuwa mtuhumiwa alikiri makosa yake na kuhukumiwa kifungo cha miezi sita gerezani au kulipa faini ya Shilingi 100,000 ambapo alishindwa kulipa faini hiyo na hivyo anatumikia kifungo kwenye gereza la Isanga kuanzia Machi 13, mwaka huu.

1 comment:
Sasa kama anamiaka 20 leo, aliwezaje kuingia Tanzania mwaka 1992? Au aliingia akiwa na umli wa mwezi mmoja?
Post a Comment