ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, April 5, 2012

NAOMBA KURA YAKO

Ndugu zangu wa DMV,

Napenda kuwajulisha kwamba mimi ndugu yenu Iddi  Sandaly, kuwa nagombea nafasi ya Kuwa Rais wa jumuia yetu ya watanzania  hapa DMV.

Kama wengi wenu mnavyonifahamu ni kwamba tumeshirikiana wote katika mambo mbali mbali  na mnanijuwa kiundani kabisa ni jinsi gani nilivyo na pia mnazifahamu sifa zangu zikiwemo za uongozi.

Lengo langu ni kuwa kiongozi ambaye nitatetea masilahi ya Watanzania wote waishio hapa DMV.

Kama tujuavyo jumuia yetu ya watanzania hapa DMV imekuwa ikikumbwa na mawimbi ya dharuba za uongozi. Nadhani ni muda na ni jukumu letu kuifufua jumuia hii na kukiimarisha chombo hichi cha DMV.

NAOMBA KURA YAKO.


Uchaguzi utafanyika siku ya Jumapili; Tarehe 15, April 2012. 

Muda 2.00PM

Mahala; Mirage Hall, 1401 University Blvd, Hyattsville, MD 20783


Nakuomba USIKOSE NA wajulishe wengine

Wenu
Iddi Sandaly.

12 comments:

Anonymous said...

Homgera sana Idd kwa ujasiri huo. Naomba utumie jukwaa hili kutuelewesha nini kuliukumba uongozi uliopita, na kama ukichaguliwa utafanya nini ili hali hiyo isijirudie?

Bagasa said...

Kaka Idd,

vizuri umejitokeza kiuwazi zaidi na umeonyesha mfano wa namna yake. HONGERA! Ila ingekua vizuri zaid ukielezea kiufupi ni MASILAHI gani utatetea.

Nimependa kuona umejiweka wazi in advace- Safi sana kaka.

Anonymous said...

wewe wacha uongo maslahi gani utatupa kwanza atukujuwi mbona ??

Anonymous said...

swali wewe ni kiongozi ya jumuiya ya waislam Tamco na mimi ni muislam nikitu gani uliweza kufanya na kuiongoza Tamco mpaka leo tukupe kura zetu naomba tuelezee vizuri tuu ili nikuelewe wewe kama mwenyekiti wa Tamco asante??

Anonymous said...

Mr sandaly,kwa jinsi ninavyokufahamu na jinsi ulivyo na (good leadeship stayle)Nina Imani sisi wana DMV tutanufaika sana kama ukowa rais wa jumuiya yetu. Nakushukuru kwa kuwa mstari wa mbele kujitokeza kuifufua jumuiya yetu iliyokua (half or dead)kwa muda mrefu sasa naahidi kukupa kura ya ndio. Na umefanya vizuri kuondoa ( doudt)na umetumia uhuru na demokrasia ya kweli.

Mdau Washington

Anonymous said...

usikonde.all the best !! na ukipata utetee kweli maslahi yetu maana mmmhh !!kilio changu sponsorship kwa wanavyuo wa Tanzania hapa USA!!

Anonymous said...

Iddy usituletee uongo kwani wewe hii jumuiya ulishawahi kufanya nini zaidi ya kusaidia Tamco kama mwenyekiti wala hatukuoni kwenye shida za watanzania wowote wewe ni mtu wa kupendelea dini tuu tunataka mtu ambae hataangalia mambo ya dini nafikiri wewe baki na Tamco sisi tunataka kiongozi ambae atatuletea maelewano wewe unafanya utenganishi mkubwa mimi nipo tamco nakufahamu na unaleta utanzania na uzanzibari sasa ukiwa kwenye jumuiya hii utatuvuruga samahani ni ushauri kiongozi wetu wa tamko!!

Anonymous said...

kwa ufupi tuu tunataka mtu ambae yupo kwenye mitazamo ya aina zote wewe umekuwa kiongozi wa dini ya kislam sasa huku kwenye jumuiya inakuje sijakuelewa point zako ??sikujuwi sana isipokuwa huku kwenye jumuiya ni vyema kabisa ungeacha nako maana hautapaweza kwa ushauri tuu

Anonymous said...

mama yangu wana dmv mumekwisha!

Anonymous said...

sasa wewe mbona hata ujanyoa hizo ndevu muheshiwa raisi?khaaa

Anonymous said...

Sasa wewe uko kwenye jumuiya ya waislamu.howcome unataka uenyekiti wa chama cha Watanzania?ili hali unajua kwenye jumuiya ya wa-Tz huwa kuna sherehe,pati za kunywa pombe,muziki na sherehe kubwakubwa na wewe ni mwenyekiti wa waislamu,unadhani hii ni kitu kizuri?labda uachie uislamu uje kwingine,sijui nani amekushauri, sasa imekaaje hii?mimi kwa mtazamo wangu naona hiki cheo hakikufai.

Anonymous said...

mbona kwenye maparty ya pombe yote anakuwepo au wewe humuonagi?