ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 17, 2012

SHUKRANI KWA WANA JUMUIYA

Katibu Amos Cherehani
WANAJUMUIYA,
Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru sana kwa maamuzi yenu makini ya kunichagua mimi kuwa mwakilishi wenu kwenye chombo hiki kinachounda Jumuiya ya Watanzania hapa DMV. Aidha , napenda kuwapongezeni sana kwa kuwa watulivu na wavumilivu katika kipindi chote cha kampeni, upigaji kura na kisha kutangazwa kwa matokeo na kila mmoja wetu kukubali matokeo.
Baada ya tukio hilo la kihistoria kuwa limekamilika, kinachofuatia sasa ni kazi ya kutimiza yale yote tuliyoahidi kama viongozi kwamba tuingeyafanyia kazi. Kazi hii ni ngumu na inahitaji sisi sote kama Watanzania tuwe tayari kujitoa kwa hali, mali, mawazo pamoja na nafsi zetu ili kuhakikisha kuwa Jumuiya yetu inasimama kama chombo kilicho imara kitakachowaunganisha Watanzania  hapa DMV na kisha kuvuka mipaka  huko Tanzania ambako tumetokea.
Kwa haya machache nasema asanteni sana na mimi nipo tayari kupokea mikoba ya Ukatibu wa Jumuiya ya Watanzania hapa DMV.
ASANTENI SANA.
Amos Matali Cherehani.
KATIBU MTEULE

No comments: