Dominique Strauss-Kahn, mkuu wa zamani wa Shirika la Fedha Duniani, IMF, anasema anaamini kashfa iliyomuandama baada ya kashfa iliyohusu mapenzi, ilichochewa na watu waliohusika na rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy.
Bwana Strauss-Kahn alijiuzulu baada ya kutuhumiwa kumbaka mfanyakazi wa hoteli mjini New York.
Hakusema kama alitegwa kukumbana na msichana huyo, lakini anadai kuwa matukio yaliyofuata yalikuwa njama ili kuhakikisha kuwa anaaibika hadharani.
Kabla ya kashfa hiyo, Bwana Strauss-Kahn akitarajiwa kumpinga Bwana Sarkozy kuania urais.
Mwandishi wa BBC anasema mahojiano hayo yametoka wakati tete, juma moja tu kabla ya duru ya pili ya uchaguzi wa rais.
No comments:
Post a Comment