ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, April 28, 2012

Tundu Lissu ‘aibuka kidedea’

Gasper Andrew,
Singida 
MBUNGE wa Singida Mashariki (Chadema),Tundu Lissu,imeshinda katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi.

Hatua hiyo imekuja baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Singida, kutupilia mbali hoja 11 zilizowasilishwa na walalamikaji katika kesi hiyo ya kutaka kutenguliwa kwa  ushindi wa Lissu kwa madai kuwa, alikiuka sheria na taratibu za uchaguzi.


Kesi hiyo ilikuwa imefunguliwa na Shabani Selema na Pascal Halu ambao ni wanachama wa CCM na wakazi wa Kijiji cha Makiungu, katika Tarafa ya Mungaa.

Akitoa hukumu hiyo jana, Jaji Mosses Mzuna wa Makahama Kuu Kanda ya Moshi alisema ushahidi uliotolea na upande wa walalamikaji, umeshindwa kuthibitisha kuwa, walalamikiwa walivunja au kiuka sheria, taratibu na kanuni za uchaguzi na kusababisha uchaguzi huo kutokuwa huru na wa haki.

Jaji huyo alisema hoja zote 11 zilizoletwa na walalamikaji, zimeonyesha ushahidi wa kuhisi,kusikia na kushuku, ambao hauna uhalisia wa mambo.

Jaji Mzuna alisema mahakama haiwezi kutegua matokeo ya uchaguzi kwa kuambiwa maneno matupu bila wahusika kuthibishwa kwa vielelezo.

Alisema ushahidi wa upande wa walalamikaji pia hakunyooka na hivyo, kushindwa kuwaunganisha walalamikiwa na tuhuma zilizokuwa zinawakabili.


Jaji Mzuna alitaja baadhi ya hoja ambazo walalamikaji waishindwa kuthibitisha kuwa ni pamoja na ile ya madai kuwa Tundu aliandaa barua tano zinazofanana kwa mawakala wa CUF,TLP,AAPT Maendeleo,NCCR -Magezui na Chadema.

"Katika hoja hii,hakuna barua hata moja yenye saini ya Tundu wala hakuna mtu aliyemwona Tundu akiziandaa au akisimamia uandaaji wa barua hizo.Barua zote lilikuwa na mihuri na saini ya makatibu wa vyama husika, "alisema 

Alisema hoja nyingine ambayo walalamikaji wameshindwa kuthibitisha ni ile ya kuwa Tundu aliwapa chakula mawakala wa chama chake na wa vyama vingine isipokuwa wa CCM,kitendo ambacho kiliashiria ni hongo ili mawakala wasiokuwa wa chama chake,nao wampigie kura.

Jaji huyo alisema kuwa wakati umefika sasa kwa watu wanaotarajia kufungua kesi za kupinga matokeo ya uchaguzi, kutambua kuwa kesi hizo sio rahisi kama wanavyofikiri,


Kwa upande wa mahakama,alisema zinapaswa kuhakikisha kuwa hazibariki hoja ambazo zina mwelekeo wa kuwanyima haki wananchi  viongozi wanaowataka.

Kesi hiyo iliyoanza machi 12 mwaka huu ambapo walalamikaji walileta mashahidi 24 kati ya 54 waliokuwa wanatarajiwa kutoa ushahidi.
Kwa upande wa Tundu,alileta mashahidi watatu na yeye wa nne.


                                                            Mwananchi

No comments: