ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, May 2, 2012

PRINCESS LEYLA'S PROM

Leyla Bezuidenhout kama kitambulisho kinavyoonyesha akiwa amemaliza High School katika shule ya Peachtree Redge iliyopo Jijini Atalanta, Georgia, Nchini Marekani 
Jiji na Atlanta linavyoonekana katika picha kutoka chumbani kwenye Hotel ya Westin iliyopo katikati ya jiji la Atalanta.
Leyla akiandaliwa na mama yake Linda Bezuidenhout Mali kwenye hii siku yake maalum ya kusherehekea kumaliza High School ndani ya chumba kwenye Hotel ya Westin.
Linda na wanae wakiwa tayari kwenye siku hii maalum ya Leyla ambayo kabla ya kwenda Dinner walivinjali mitaa ya Atlanta kwa Farasi.
Leyla (Tanzania Cinderella) na mama yake wakielekea kupanda
Leyla na familia yake wakiwa kwenye Farasi
Leyla akiwa na mzazi wake Mr. Mali
Leyla akisaidiwa kushuka kwenye Farasi baada ya kuvinjali katikati ya jiji la Atlanta
Leyla na mama yake Linda wakipiga picha ya pamoja nje ya Hotel ya St. Regis jijini Atalanta, Georgia.
Leyla akipata picha ya kumbukumbu katika siku yake maalum nje ya Hotel ya St. Regis.
Linda akimrekebisha mwanae kabla ya chakula cha jioni kwenye Hotel ya St. Regis.
Leyla akiwa kwenye Dinner.
Leyla akiwa na wanafunzi wenzake hafla ya kusherehekea kumaliza High school iliyofanyikia Fox Theater.

14 comments:

Anonymous said...

Umependeze Leyla. Hongera sana. Ila nguo haiwndani na sherehe

Anonymous said...

elimu ni ufunguo wa maisha, use it wisely. congrats

Anonymous said...

Kapendeza sana kawaida ya prom ni shughuli ilio so formal. Wavulana uvaa Tuxidos na wasichana nguo nzuri utakayo nguo za Cinderella ndo zinakuwa na soko kubwa kipindi cha prom naona mwenzie kapiga Cinderella lakini yake fupi. Walipendeza kwakweli. Big up sister Lindah.

Anonymous said...

kwani anaolewa au prom nguo hapana mhh haiendani na shughuli yenyewe

Anonymous said...

Yaani kumaliza High school tu unataka kung'aa kama malkia je ingekuwa ndio umegraduate na PHD je?

Anonymous said...

Hongera kwa kumaliza high school. uendelee hadi PHD !!Inshallah !!
Linda mzuri jamani aaahhh ! I like her so much !!

Anonymous said...

http://www.newyorkdress.com/Prom_Ball_Gowns.html wadau msiojuwa dress code ya nguo za prom ingieni hapo au google " prom dresses" hii ni perfect kwa prom ball gown.

Anonymous said...

Jamani msiojuwa nguo za prom zikoje nendeni google. Kalagenibao ngojeeni watoto zenu wakikuwa mwape jeans on their prom day. Kama hamkuchekwa. Naisi akipata PHD itakuwa kushinda hivi. Tuombe maisha marefu mtoto wa dada lao la mujini daresalama. mlitegemea atapelekwa Mc Donald's?

Anonymous said...

Akipata PHD atakuwa kubwazima hapa anadekezwa mwisho mwisho acheni ushamba jamani. Kwani haka ni katoto jamani hata kitoto mna kihate? Mwanae wa kwanza huyo mwacheni amdekeze kwani si mmezaa dekezeni wenu na nyinyi. Haloooo kazi yenu kununua miviatu na minywele mnasahau watoto zenu wacheni wanaojuwa kulea wafanye vitu vyao.

Anonymous said...

Hii kweli kazi!high school hivi tu!je PHD?na ujitahidi ufike usione ujanja kusheherekea High school diploma ambayo ni nothing nowdays!kweli nguo ni (overdressing)sio wivu bali iukweli,shughuli yenyewe na nguo mmmmmhhh!!!!.but umemuwakilisha mwanao,katika siku yake muhimu.

Anonymous said...

Mjomba hili jina la Mwisho huna lina nishinda kutamka ni bezutehuti? kizungu kigumu,mwe!
Ni mimi -Mwakifulefule-Tukuyu mbeya

Anonymous said...

Mmeshaambiwa ni princess mlitegemea iweje? Someni kichwa cha habari mlitaka avalishwe Dira? Na mafuta ya nazi yenye karafuu.

minisha said...

mamaaa jaman nguo ya prom inatakikana iwe kama aliyovaa leyla na friends wake ni inatakikana iwe ya partyy hamjuii hapo nyamazeni tuu kazi kumpondaa kumbe hamjui nguo zinavotakikana zivaliwee tembeeni muonee loohh leyla a lovee it yu look beutifull dearrr muahxxxxxxx fabolous <3

Anonymous said...

Kapendeza...phd itakua kubwa kuliko hii kwa raha zako misez mali tuombe uzima uzidi kumfurahisha bintio..