Joseph Zablon
PAMOJA na kutolewa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, Simba iliwasili jana mchana jijini Dar es Salaam toka Sudan na kupokewa kwa mbwembwe na mashabiki wa timu hiyo, huku Kocha Cirkovic Milovan akijitetea kwa kusema wapinzani wao wamesonga mbele kwa sababu tu bahati ilidondoka upande wao.

Simba ilitua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa J.K Nyerere na ndege ya Shirika la Ndege la Kenya , KQ315 na kupokewa na kundi kubwa la mashabiki wakiongozwa na kikundi cha matarumbeta cha Kidedea.
Wekundu hao wa Msimbazi walitolewa kwa mikwaju ya penalti 9-8 na Al Ahly Shandy baada ya kufungwa mabao 3-0 katika mchezo wa marudiano, na hivyo kufanya matokeo kuwa 3-3. Katika mchezo wa kwanza, jijini Dar es Salaam, Simba ilishinda 3-0.
Mara baada ya kuwasili, Kocha Circovic alisema kikosi chake kilijitahidi kucheza kufa na kupona kwenye mchezo huo mgumu wa ugenini, lakini bahati hakikuwa yao.
"Katika soka kuna matokeo matatu, kushinda, kufungwa na kutoka sare. Sisi tulijitahidi kadri tulivyoweza lakini, uzani wa matokeo haukulala upande wetu. Nimekubali matokeo, tunajipanga kujipanga kwa ajili ya michuano mingine ya kimataifa," alisema Milovan.

Milovan aliwashukuru mashabiki wa Simba kwa kuonyesha mapenzi makubwa na sapoti ya kutosha wakati wote wa maandalizi ya mchezo huo wa marudiano na hata waliporejea.
"Sikutarajia mapokezi kama haya toka kwa mashabiki, kweli hii inaonyesha mashabiki wana mapenzi na timu yao. Tumerudi bila ushindi, lakini tumepokewa kama mashujaa," alisema zaidi.

Mwenyekiti wa klabu hiyo, Aden Rage alisema makosa matatu waliyofanya katika mchezo huo yamewagharimu na wanayakubali matokeo na hivi sasa mtazamo wao ni katika mechi zaidi za kimataifa.
"Hivi sasa tunaiangalia michuano, mapokezi tuliyopewa yanaonyesha ni jinsi gani washabiki wetu walivyo watu wa mpira," alisema Rage.

Kipa Juma Kaseja alisema kilichotokea ni mambo ya kawaida katika mchezo wa soka. "Nina imani kocha amebaini makosa yaliyotokea na atafanya marekebisho kwani tuna mashindano mengine ya kimataifa mbele yetu."
"Tumecheza vizuri kadiri na uwezo wetu na matokeo yamekuwa kama ulivyosikia, lakini ni mambo ya kawaida na ninaamini kocha na viongozi watakuwa wanapanga mipango ya mambo mengine ya mbele," aliongeza Kaseja.

No comments:
Post a Comment