Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoani Mwanza inamshikilia Ofisa Utumishi Mkuu Daraja la Pili katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Pius Songoma, kwa tuhuma za kuomba rushwa ya ngono kutoka kwa mwalimu mmoja wa kike (jina linahifadhiwa).
Kamanda wa Takukuru Mkoani Mwanza, Christopher Mariba, alisema jijini hapa jana kuwa, Ofisa Utumishi huyo alikamatwa juzi wakati akiwa katika harakati za kutekeleza azma yake hiyo katika gesti bubu moja iliyopo maeneo ya Mkuyuni.
Akizungumzia chanzo, mazingira hadi kukamatwa kwa Ofisa Utumishi huyo, Mariba, alisema kwamba ofisi yake ilipokea taarifa kutoka kwa mwalimu huyo siku kadhaa zilizopita, hivyo wakaamua kuweka mtego wa kumnasa mtuhumiwa.
Kwa mujibu wa Mariba, Mwalimu huyo alipata uhamisho kutoka Shule ya Sekondari iliyopo wilayani Kwimba kwenda katika shule moja ya sekondari iliyopo jijini Mwanza.
Alisema mwalimu huyo alikuwa akiomba uhamisho wa kwenda Mwanza ili kuwa katika mazingira mazuri ya kuwalea wadogo zake baada ya wazazi wake wote wawili kufariki dunia.
Hata hivyo, alisema kwamba baada ya kuwa amefuata taratibu zote ikiwa ni pamoja na kuripoti kituo cha kazi, mwalimu huyo alikwenda pia kwa ofisa utumishi huyo kwa ajili ya kujaziwa fomu zinazofahamika kama “data sheet” ili kukamilisha zoezi hilo.
Mariba alisema kuwa tangu mwanzo baada ya kupokea fomu hizo, mtuhumiwa alionyesha dalili zote za kumtaka mwalimu huyo kingono ndipo amjazie fomu hizo.
“Hali hiyo ilimnyima raha huyu mwalimu, ndipo akaamua kutafuta ushauri kwa rafiki zake kabla ya kuja kwetu kutupatia taarifa na kisha tukaweka mtego ambao ulisaidia kumnasa mtuhumiwa,” alisema.
Aliongeza kwamba, awali ilikuwa wamkamate mtuhumiwa huyo Jumatatu iliyopita katika Hotel ya City iliyopo Kirumba, lakini waliahirisha operesheni hiyo kutokana na mazingira kutokuwa mazuri kufanikisha kazi hiyo.
Hata hivyo, alieleza kwamba hatimaye juzi (Jumatano) waliweka mtego mwingine ambapo mtuhumiwa na mwalimu huyo kwa maelekezo ya maofisa wa Takukuru walikubaliana kukutana katika mgahawa wa Pizzeria, na kwamba baada ya kukutana hapo Songoma aliacha gari lake na kuchukua gari la rafiki yake kuekelea eneo la tukio.
Ofisa huyo wa Takukuru alisema kuwa wakati hayo yakiendelea maofisa wawili wa kike wa Takukuru walikuwa wakifuatilia nyendo zote hizo kuanzia Pizzeria hadi Butimba na kisha kurejea Mkuyuni hadi katika gesti bubu moja ambayo haina jina.
“Kimsingi, tulijipanga vizuri sana, tuliwatumia maofisa wetu wa kike ndio walioweza kumkamata huyu jamaa akiwa tayari ameingia chumbani tayari kwa kufanikisha azma yake hiyo,” alisema.
Aliendelea kusema kwamba baada ya kumkamata na kumhoji mtuhumiwa, alidai kuwa alikwenda hapo kwa majukumu ya kikazi, utetezi ambao hata hivyo Takukuru waliupuuza kwa sababu tayari walikuwa na taarifa za kutosha.
Mariba alibainisha kwamba wameshapokea malalamiko mengi kuhusu mtuhumiwa huyo kushawishi rushwa.
Alitoa ushauri kwa watu wengine kuwa jasiri kama mwalimu huyo ili kufanikisha vita dhidi ya rushwa miongoni mwa watumishi wa umma na sekta binafsi.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment