Watanzania wa DMV, uongozi wetu umewaomba mtengeneze kamati, ili ziweze kuchambua na kufuatilia kwa kina mambo ya maendeleo ya Jumuiya na watanzania kwa jumla. Kamati kwa mfano ile ya fedha ipate wataalam watakaofuatilia kupata pesa za kuisaidia Jumiya yetu kujiendesha, na ile ya uhamiaji kujaribu kufuatilia namna ya kuwawezesha watanzania hapa kupata makaratasi, kutoa ushauri wa namna ya kupambana na kesi zinazohusu makaratasi, ajira, na shule. Mimi ninavyoona ni jambo zuri sana Jumuiya imeanza vizuri lakini isipopata ushirikiano, nao itapigwa mweleka na kulala chali kama zilivyokuwa zile Jumuiya zilizopita. Watanzania jitokezeni kwa wingi ili tuisaidie Jumuiya yetu kuunda chombo madhubuti kwa ajili ya manufaa yetu wenyewe. Bila sisi kusimama kidedea kuisaidia Jumuiya yetu basi kura zetu zitakuwa hazina maana yeyote. Prezidaa wa Jumuiya ameshaanza kulalamika kwamba watu hawajitokezi, sasa sijui tuelewe nini? Lazima sasa kama wana DMV tukubali kufa kwa ajili ya Jumuiya vinginevyo tuiache ife kifo cha Sadam Huseein. Nawasilisha.
1 comment:
Watanzania wa DMV, uongozi wetu umewaomba mtengeneze kamati, ili ziweze kuchambua na kufuatilia kwa kina mambo ya maendeleo ya Jumuiya na watanzania kwa jumla. Kamati kwa mfano ile ya fedha ipate wataalam watakaofuatilia kupata pesa za kuisaidia Jumiya yetu kujiendesha, na ile ya uhamiaji kujaribu kufuatilia namna ya kuwawezesha watanzania hapa kupata makaratasi, kutoa ushauri wa namna ya kupambana na kesi zinazohusu makaratasi, ajira, na shule. Mimi ninavyoona ni jambo zuri sana Jumuiya imeanza vizuri lakini isipopata ushirikiano, nao itapigwa mweleka na kulala chali kama zilivyokuwa zile Jumuiya zilizopita.
Watanzania jitokezeni kwa wingi ili tuisaidie Jumuiya yetu kuunda chombo madhubuti kwa ajili ya manufaa yetu wenyewe. Bila sisi kusimama kidedea kuisaidia Jumuiya yetu basi kura zetu zitakuwa hazina maana yeyote. Prezidaa wa Jumuiya ameshaanza kulalamika kwamba watu hawajitokezi, sasa sijui tuelewe nini? Lazima sasa kama wana DMV tukubali kufa kwa ajili ya Jumuiya vinginevyo tuiache ife kifo cha Sadam Huseein.
Nawasilisha.
Post a Comment